Home Habari za michezo KUHUSU AZIZI KI….GAMONDI NAYE KATIA NENO LAKE….AMTAJA MESSI….

KUHUSU AZIZI KI….GAMONDI NAYE KATIA NENO LAKE….AMTAJA MESSI….

Habari za Yanga leo

Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi afichua alichomwambia Stephanie Aziz Ki kuhusu mbio zake za kusaka ufungaji bora msimu huu akisema kuwa kiungo huyo ni mchezaji hatari na muhimu ndani ya kikosi chake.

Gamondi amesema hayo baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya NBC huku Yanga wakibeba Ubingwa na Aziz Ki akiibuka mfungaji bora na mabao 21 na kuongeza kuwa, Aziz ni kama Lionel Messi.

“Ninajivunia kuwa naye, nilimwambia mwanzoni kabisa mwa msimu kuwa unaweza kuwa mfungaji bora kwa sababu ni mchezaji mzuri. Sio Aziz tu bali timu nzima imepambana sana.

“Mwanzo wakati nazungumza na raisi kabla sijajaja hapa nilikua alikua akitafuta number 10 nilimwambia una (Black Messi) Messi Mweusi hapa kwa sababu nilikua naangalia video za Aziz ki ni kama Messi pamoja na heshima zote kwa Messi. Anaeweza kushinda mechi na kutengeza nafasi. Anaweza akashika mpira mara chache ndani ya dakika 90 lakini ni mchezaji hatari.

“Tumekuwa na msimu bora sana, kupata alama 80 na kufunga mabao ya kutosha, tulikuwa bora kwenye kushambulia na bora kwenye kujilinda ninadhani tuliwaacha mbali sana wengine, tumekuwa timu bora. Ninawapongeza sana kila mmoja sio Aziz tu, sawa Aziz amefanya jitihada kubwa lakini kwa kusaidiwa na wachezaji wote kwenye timu,” amesema Gamondi.

SOMA NA HII  ONANA AJICHIMBIA KABURI MWENYEWE MSIMBAZI