Home Habari za michezo UGUMU KUTOKANA NA UWEPO WA LOMALISA WAMFANYA KIBABAGE KUFUNGUKA HAYA YANGA….

UGUMU KUTOKANA NA UWEPO WA LOMALISA WAMFANYA KIBABAGE KUFUNGUKA HAYA YANGA….

Habari za Yanga leo

Beki wa kushoto wa Yanga, Nickson Kibabage amesema anafurahia kuwa miongoni mwa kikosi cha ushindi cha timu hiyo ingawa kutopata nafasi kwenye kikosi cha kwanza imekuwa ikimtatiza.

Kibabage aliyejiunga na Yanga msimu huu akitokea Singida Big Stars amekuwa akikutana na changamoto ya nafasi ya kudumu dhidi ya Joyce Lomalisa na winga Farid Mussa.

Wachezaji hao wawili mara kadhaa nao wamekuwa wakitumika katika eneo la ulinzi wa kushoto na hivyo kuongeza ushindani katika kikosi cha kwanza.

“Mimi ni mchezaji wa Yanga, nafurahia hilo kwani bado nitaendelea kuwepo hapa lakini kikubwa kwenye timu yetu mtu yoyote huwa anacheza, ukipata nafasi unajitahidi kufuata maelekezo ya kocha kwa lengo la kuhakikisha timu inapata matokeo.

“Changamoto zipo mfano ugumu unakuja labda pale unakuta upo kwenye muendelezo na kiwango thabiti na halafu mechi inayokuja unaambiwa huchezi, kwa hiyo kwa namna moja ama nyingine inakuwa kama inakukata kidogo,” alisema Kibabage.

Beki huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar na Difaa El Jadida ya Morocco hata hivyo amesema ataendelea kupambana kila anapopata nafasi ili aendelee kuwa miongoni mwa mafanikio ya timu lakini pia kuzifikia ndoto zake.

SOMA NA HII  SIKU CHACHE BAADA YA KUWA MCHEZAJI WA KWANZA KUTEMWA....MORRISON NAYE AANZA KUJIBU MAPIGO KWA SIMBA...