Home news MANARA AENDELEA ‘KUTEMA NYONGO’ MSIMBAZI, SAFARI HII KAJA NA HILI…

MANARA AENDELEA ‘KUTEMA NYONGO’ MSIMBAZI, SAFARI HII KAJA NA HILI…


Aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, amewashukia wanaoendelea kuendesha kampeni ya wadau wajiondoe kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Manara amewajibu wanaoendesha kampeni hiyo kwa kupost bango linalosisitiza kampeni kwa wadau, kwenye kurasa zake huku akisistiza kuwasaidia kwenye kampeni hizo.

SOMA PIAWAKATI LUIS AKIIBUKIA AL AHALY… MUGALU HUYOO APATA SHAVU TIMU KUTOKA MOROCCO

Manara ambaye jana aliongea na wanahabari jijini Dar es salaam na kuacha taharuki kubwa kwa wadau wa soka, ameandika: “Labda wanadhani mimi ni dhaifu Kwa hizi kampeni zao uchwara.”

“Guys kipi kinawasubirisha humu? Waambieni waliowatuma Mungu ndio Alfa na Omega..”

“Badala ya kujibu hoja mnaleta vioja? Sasa nawasaidia kuwapostia..Haya potea fasta Mtatoka kumi wanakuja buku wapyaaaaaaa

Naitwa Bugatti!!Gastadialo”

SOMA NA HII  KUHUSU MECHI YA KESHO....NABI AJIAPIZA JAMBO YANGA...REAL BAMAKO WAINGIA MCHECHETO...