Home Yanga SC BREAKING: AUCHO ATAMBULISHWA RASMI YANGA, AFUNGUKA

BREAKING: AUCHO ATAMBULISHWA RASMI YANGA, AFUNGUKA


RASMI: UONGOZI wa Yanga leo Agosti 9 umemtangaza nyota mpya Khalid Aucho, winga kutoka nchini Uganda.

Nyota huyo alishuka Tanzania usiku wa kuamkia leo kisha akamalizana na timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu,  Nasreddine Nabi. 

Ni miaka miwili amesaini kwa ajili ya kuitumikia timu ya Wananchi ambayo inashiriki michuano ya kimataifa msimu ujao.

Ligi ya Mabingwa Afrika ni michuano ya kimataifa ambayo Yanga itashiriki baada ya Tanzania kupata nafasi nne za kupeleka timu na timu hiyo ilimaliza ikiwa nafasi ya pili kwenye ligi.

Aucho amesema:”Malengo ya kila mchezaji ni kucheza timu kubwa, Yanga ni timu kubwa hivyo kwa sasa mimi ni njano na kijani,” .

SOMA NA HII  GAMONDI:- "KATIKA MAISHA USIJIAMINISHE SANA...BADO TUNA GEPU KUBWA...AMEFUNGUKA HAYA