Home Yanga SC KABWILI ABAKI, SHIKALO NA METACHA MNATA PANGA LIMEWAKUTA

KABWILI ABAKI, SHIKALO NA METACHA MNATA PANGA LIMEWAKUTA


 UONGOZI wa Yanga umetangaza kuachana na makipa wao wawili ambao walikuwa ndani ya kikosi hicho kwa msimu wa 2020/21.

Ni Metacha Mnata na Faroukh Shikalo ambao walikuwa wakipishana langoni kwa msimu uliopita.

Kipa namba tatu Ramadhan Kabwili atabaki ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na kocha Razack Siwa kwa makipa.


Kabwili alidaka mchezo mmoja ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21 ambapo ilikuwa mbele ya Dodoma Jiji.

Hii ni kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa.

SOMA NA HII  KWA HILI GAMONDI KAZI ANAYO HUKO YANGA