Home Habari za Simba Leo MGUNDA AMTABIRIA MAKUBWA JOHN BOCCO…”UKIMUULIZA ATANITAJA”

MGUNDA AMTABIRIA MAKUBWA JOHN BOCCO…”UKIMUULIZA ATANITAJA”

JOHN BOCCO

EL CAPITANO PAPAA John Bocco, Jina kubwa kuwahi kutokea kwenye ardhi ya Tanzania, Mitaa ya Msimbazi inamfahamu kwa mabao yake matamu, Mitaa ya Chamanzi kwa watoto wa kishua, Azam FC picha ya nyota huyu inatakiwa waitafutie Fremu ya picha.

John Boco baada tu ya msimu wa 2023/24 kuisha alitanganza rasmi kuachana na kucheza soka la kulipwa, na hivyo kuendelea na maisha yake mengine nje ya uwanja kama kocha wa timu za vijana wa Simba SC.

Gwiji huyu wa kufumania nyavu za wapinzani amedumu kwa miaka saba kwenye kikosi cha Simba baada ya kujiunga msimu wa 2017/18 na kutwaa mataji manne ya Ligi Kuu, FA mawili.

Pia ameisaidia timu yake kucheza robo fainali tano za michuano ya CAF, nne zikiwa za Ligi ya Mabingwa Afrika na moja ya Kombe la Shirikisho.

Kaimu kocha Mkuu wa Simba Juma Mgunda amemuelezea kwa undani zaidi, mchezaji John Bocco huku akisisitiza kwamba alimshauri kusomea ukocha.

“Ukimtafuta na kumuuliza kuwa nani alimshauri asomee ukocha atanitaja. Ni kijana wangu mbali na kumfundisha amekuwa muungwana, msikivu. Namtabiria kuwa atakuja kuwa kocha bora miaka ujayo,” alisema.

“Bocco ni mchezaji kiongozi na ndio maana mara nyingi timu alizopita alikuwa nahodha kwa sababu ni mchezaji ambaye anaweza kuishi na kila mtu na ni mwepesi wa kuelekeza mtu akaelewa.”

Mgunda alisema Bocco ni mchezaji ambaye ataendelea kuishi mioyoni mwa Taifa na sio Simba tu kwa sababu mambo makubwa aliyoifanyia hii nchi sio kwa upande wa klabu tu bali hadi timu ya taifa ‘Taifa Stars’

SOMA NA HII  GAMONDI AGEUKA KIVURUGE KWA WAPINZANI