Home Habari za Yanga Leo WALICHOSEMA AZAM FC KABLA YA MCHEZO WA FAINALI NA YANGA SC

WALICHOSEMA AZAM FC KABLA YA MCHEZO WA FAINALI NA YANGA SC

azam fc

Afisa Habari wa AZAM FC Hasheem Ibwe amewapiga mkwara mzito Yanga SC kuelekea mchezo wa fainali, Kombe la Shirikisho huko Zanznbiar.

Mchezo huo wa Kombe la Shirikisho la CRDB unatarajiwa kuchezwa leo Juni 2 2024 Uwanja wa New Amaan Complex, Baada ya Uongozi kusema wanautaka mchezo huo.

Uongozi na wachezaji wa timu hiyo wamesema kuwa hii ni karata muhimu zaidi kwao ya kuhakikisha wanaumaliza msimu wakiwa na taji mkononi na hivyo watapambana kufa na kupona.

Ikumbukwe kwamba Azam FC kwenye fainali ya 2022/23 walipoteza Uwanja wa Mkwakwani, Tanga baada ya kushuhudia ubao ukisoma Azam FC 0-1 Yanga na bao pakee la ushindi lilifungwa na Kennedy Musonda.

Ofisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe ameweka wazi kuwa wanachukulia fainali kwa umakini na wanatambua umuhimu wa kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wao.

“Tuliweka wazi tangu awali kwamba tunahitaji kufanya vizuri hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi tupo tayari kwa ajili ya kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wa fainali.”

Msimu huu Azam FC wamekuwa na kiwango  bora sana, wamefanikiwa kumaliza katika nafasi  ya pili kwenye msimamo wa Ligi kuu, na hivyo inawapa nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2024/25

Anayetazamwa sana leo kubadilisha matokeo kwa upande wa Azam FC ni Feitoto,  ambaye amekuwa na kiwango kizuri kwa msimu huu kwenye Ligi Kuu pekee alifunga mabao 19. Je atawafunnga tena kwa mara pili baada ya kufanya hivyo kwene mchezo uliopita wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu.

SOMA NA HII  DIARA AZIDI KUIPAISHA JUU LIGI YA TANZANIA...AITWA TENA MALI KWA KOMBE LA DUNIA...