Home Habari za Yanga Leo YANGA YAWATEGA AZAM FC…FAINALI YA KISASI ZANZIBAR

YANGA YAWATEGA AZAM FC…FAINALI YA KISASI ZANZIBAR

TIMU HIZI KUIPA UBINGWA YANGA...GUEDE AENDELEZA MAAJABU AFANYA HAYA

MUDA wa kutafutana ubaya umefika, leo Juni 2, 2024 ndiyo siku  ya fainali  ya Kombe la  Shirikisho la CRDB, kati ya Azam FC dhidi ya Yanga SC, ambapo mabingwa hao watetezi wamesema hataingia kulipa kisasi   bali watacheza kama wapo mazoezini.

Msimu uliopita Yanga SC walitwaa ubingwa wa kombe la Shirisho kwa kuwafunga Azam FC kwa bao 1-0, huko mkoani  Tanga katika dimba la Mkwakwani, na hii ndiyo  sababu ya kocha wa KLABU hiyo  Miguel  Gamondi kusema kuwa hafikirii kulipa kisasi.

Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wanatambua mchezo wao utakuwa na ushindani mkubwa ila watapambana kucheza soka safi hawafikirii kuhusu kulipa kisasi.

“Yanga ndiyo timu inayocheza soka safi zaidi Tanzania hilo lipo wazi, lakini kuelekea mchezo wetu wa fainali tupo vizuri na hatuna mpango wa kulipa kisasi kwa kuwa mchezo wa mpira hauhitaji kulipizana visasi bali maandalizi.

“Ninaamini kwamba utakuwa mchezo wenye ushindani mkubwa hilo lipo wazi tutafanya kazi kubwa kwa kuwa wachezaji wapo tayari hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi.”.

Mwamuzi wa mchezo huo wa fainali ni Ahmed Arajiga, ambaye alikuwa pia ni mwamuzi kwenye Kariakoo Dabi mzunguko wa pili uliochezwa Uwanja wa Mkapa. Na mchezo huo utapigwa majira ya saa 2:15 za Usiku katika dimba la  New Amaan Zanzibar.

Katika mechi ya mzunguko wa pili wa Ligi kuu ya NBC, uliopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa, Azam FC walibuka na ushindi wa  mabao 2-1, Je leo ngoma itachezwa zaidi na mashabiki wa timu gani?

SOMA NA HII  FEISAL SALUM "FEI TOTO" KUREJEA YANGA...MARA BAADA YA KUMALIZA MAJUKUMU YA TAIFA STARS