Home Michezo FEISAL SALUM “FEI TOTO” KUREJEA YANGA…MARA BAADA YA KUMALIZA MAJUKUMU YA TAIFA...

FEISAL SALUM “FEI TOTO” KUREJEA YANGA…MARA BAADA YA KUMALIZA MAJUKUMU YA TAIFA STARS

Habari za Yanga

Kama ulikuwa hujui basi nikujuze kuwa suala la kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ na klabu yake ya Yanga halijakwisha na litaisha pale tu mchezaji huyo atakaporejea kambini kuungana na wenzake.

Kwa sasa Feisal ameungana na wachezaji wenzake katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars’ ambacho kilitua nchini Misri siku ya jana.

Viongozi wa Yanga wamekuwa na mazungumzo na mchezaji huyo wakimtaadharisha na kumtaka arejee na kama ni masuala ya maslahi yake basi watayaweka sawa pindi atakaporejea kikosini.

Ni takribani miezi mitatu sasa tangu Feisal aondoke Jangwani akishinikiza kuvunja mkataba wake ambao unatarajiwa kumalizika mwezi May 2024.

Yanga walizima jaribio lake la kutaka kuvunja mkataba huku wakimfungulia mashtaka mchezaji huyo kwa kupeleka shauri hilo TFF na maamuzi yalieleza wazi kuwa Feisal ni mchezaji halali wa Yanga akiwa na mkataba halali na Yanga.

Fununu zinaeleza kuwa Feisal anaweza kurejea kikosini baada ya majukumu ya timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars’ na ataungana na baadhi ya wachezaji wenzake wa kikosi cha Yanga waliko pamoja.

Tangu mchezaji huyo ameondoka kikosini bado Yanga imekuwa ikipata matokeo na soka safi likichezwa na hivyo Wananchi wamekuwa hawamzingatii sana.

Ikumbukwe kuwa kama Feisal ataendelea kuweka mgomo basi anaweza kukumbana na adhabu kali.

SOMA NA HII  MFAHAMU STAA MKUBWA WA SOKA DUNIAN ANAYELIPWA BILION 26 LAKINI BADO ANAISHI KWA WAZAZI WAKE...