Home Habari za Simba Leo MURTAZA MANGUNGU ACHAFUA MSIMBAZI…KUHUSU KUHUJUMU TIMU

MURTAZA MANGUNGU ACHAFUA MSIMBAZI…KUHUSU KUHUJUMU TIMU

MWENYEKITI wa Klabu ya Simba Murtaza Mangungu amefunguku kila kitu kuhusu upande wake juu ya kile kinachoendelea katika klabu hiyo, ambapo katika kujibu maswali ya mashabiki aliyoulizwa moja ya swali lilikuwa ni kuhusu yeye kusemekana ana hujumu Simba.

Akifanya mahojiano na Clouds FM Mangungu alisema kwamba, yeye hajawahi kuihujumu klabu hiyo tangu awe mwanachama wa Simba takribani miaka 30 sasa.

“Sisi tunajuana tangu tunakua , haiwezekani mtu ambaye hana nasaba na Simba akawa ndani ya klabu , mimi nimepata kadi yangu ya uwanachama mwaka 1993”

“Niulize sasa , Kwahiyo tangu mwaka 1993 tuseme nilijipanga nije kuwa mwemyekiti wa Simba ili nije kuihujumu ? anayenishutumu mimi nahujumu Simba yeye hata kadi ya uanachama hana”

Aidha Mangungu amewataka mashabiki wa klabu hiyo kuwa watulivu kipindi hiki, viongozi wakipambana kurudisha makali ya Mnyama Simba.

“Niwatake mashabiki wa Simba kuwa watulivu kipindi hiki tunakamilisha taratibu zote, mimi sijawahi kumkataa MO Dewji hivyo tumemruhusu achague wajumbe wake na sisi tutampitisha kwenye mkutano wa wajumbe, kikatiba”

Katika kumalizia mahojiano yake Mwenyekiti Mangungu alihitimisha kwa kusema kwamba giza haliondolewi na giza.

“Kipindi tunahitaji utulivu, mashabiki wanatakiwa kuelewa kwamba, Giza haliondolewi na Giza, bali huondolewa na mwanga” Murtaza Mangungu Mwenyekiti wa Simba SC.

Murtaza Mangungu amekuwa ni kiongozi wa klabu hiyo kwa nafasi ya Uenyekiti kwa vipindi viwili tofauti, huku akiwa kachaguliwa kwa awamu ya pili ambapo ili kumuondoa madarakani inatakiwa wanachama washinikize ajiuzulu bila ya kujiuzulu yeye binafsi, njia ya pili ni kusubiri mida wake kikatiba uishe ndipo wachague mtu mwingine.

SOMA NA HII  ROBERTINHO AFURAHISHWA NA MASTAA HAWA MECHI YA JANA