Mwenyekiti wa Klabu ya Simba SC, Murtaza Mangungu, amesema mshambuliaji wao Pa Omar Jobe ana mkataba mrefu hivyo ni ngumu kuuvunja.
Mangungu amefunguka hayo kupitia kipindi cha Sports Arena cha Wasafi FM.
โMkataba wa Jobe ni mrefu kidogo sidhani kama tutaweza kuuvunja, kwanza sio mchezaji mbaya ni mchezaji mzuri na nilimtembelea, tumezungumza na tutaendelea na mchakato wa kuhimalisha kiwango chake.โ โ Murtaza Mangungu.
Hata hivyo, mapema leo hii msemaji wa Klabu hiyo Ahmed Ally amesema kuwa wataanza kutangaza majina ya wachezaji watakopigwa panga kuelekea msimu ujao.
Inafahamika kuwa kuna uwezekano mkubwa mapro wengi wakapigwa na mkono wa kwa heri kutokana na kutokidhi matarajio ya mabosi wa timu hiyo pindi walipowasajili.
Kuelekea msimu ujao inatazamiwa Simba itakuwa na sura nyingi mpya za wachezaji mapro haswa baada ya Mohammed Dewji kurejea kwenye nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi nafasi ambayo inampa uwanda mpana wa kufanya maamuzi makubwa ndani ya klabu.
Itakumbukwa kuwa msimu ulioisha, ambapo Simba hawakuwa kwenye kiwango bora wamemaliza ligi wakiwa kwenye nafasi ya tatu nyuma ya Yanga waliotwa ubingwa na Azam walioshika nafasi ya pili.