Home Habari za Simba Leo SABABU ZA MO DEWJI KUMRUDISHA MAGORI & TRY AGAIN SIMBA.

SABABU ZA MO DEWJI KUMRUDISHA MAGORI & TRY AGAIN SIMBA.

Habari za Simba leo

Mwekezaji wa Simba MO Dewji’, amefanya uteuzi wa wajumbe wa bodi wa upande wake, akiwarudisha watu wa mpira ndani ya klabu hiyo.

Akitangaza uteuzi huo, MO alisema kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa kwenye makubaliano na Simba ibara ya 40, amewateua Salim Mhene ‘Try again’,Mohamed Nassoro, Crescentius Magori,Hussein Kita, Zulfikar Chandoo na Rashid Shangazi.

Wajumbe hao wataingia kwenye bodi ya Simba wakiwa upande wa mwekezaji, ambapo ndani ya majina hayo sura tatu za Magori, Nassoro na Try again ni zile zilizokuwa kwenye bodi ya kwanza ya klabu hiyo zilizofanikisha Simba kuchukua mataji mara nne mfululizo.

Aidha, MO Dewji alisema baada ya mazungumzo ya muda mrefu, amekubali kujiuzulu kwa waliokuwa wajumbe Hamza Johari na Dk Raphael Chegeni.

“Baada ya kushauriana na Johari kwa muda mrefu, ameniomba apumzike kutokana na kubanwa na majukumu yake ya kikazi, hata hivyo nimemuomba abaki kwenye baraza la ushauri na amekubali,” amesema MO.

“Pia Mwanasimba kindakindaki Raphael Chegeni ameniomba kupumzika kwa kuwa amekuwa yupo kwenye bodi nyingi mbalimbali naye amekubali kuingia kwenye baraza la ushauri.”

sababu za Muwekezaji MO Dewji kuwarudisha watu wa mpira Msimbazi,  ikiwemo Magori ni kutokana na Simba kushindwa kufanya vizuri kwenye Ligi, na sajili mbovu kwa misimu mitatu, hali iliyopelekea kupoteza ubingwa wa Ligi Kuu na makombe mengine ya ndani.

SOMA NA HII  NGOWI:- JEZI ZA YANGA KWA MISIMU MITANO IJAYO ZIKO TAYARI.....