Kikosi cha Yanga, kinatarajia kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya kuweka kambi nchini humo tayari kwa msimu mpya wa mashindano.
Yanga imekubali ombi la klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kwenda nchini humo kwa ajili ya kucheza mechi ya kirafiki mechi inayotarajiwa kupigwa Julai 17 mwaka huu wakati wa kipindi cha maandalizi ya msimu mpya yaani Pre Season.
Akizungumza nasi jana, Afisa habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema safari hii kambi yao haitakuwa Kigamboni kama ilivyo kawaida badala yake wanaelekea Afrika Kusini.
Amesema wanaelekea nchini humo kutokana na mialiko waliyoipata na kuitumia sehemu ya Pre Season hiyo kujiandaa na mashindano yaliyolo mbele yao kwa msimu ujao.
“Safari hii tunakuja tofauti na misimu ya nyuma, tunatarajia kuweka kambi Afrika Kusini, kwa mwaliko wa klabu mbalimbali na tunatakiwa kwenda Kenya kwenye ufunguzi wa uwanja wa Kisumu.
Tunatarajia kufanya ziara kwa mataifa yote tuliyoalikwa kwenda na ‘Pre Season‘ yetu itakuwa Afrika Kusini itakuwa ni sehemu tulivu kwa ajili ya maandalizi ya kikosi chetu,” amesema.
Kamwe amesema wanaimani itakuwa pre seasons nzuri kwa sababu watapata mechi za kirafiki zenye ushindani mkubwa kujianda na msimu wa 2024/25.
Takriban misimu mitatu Yanga hawakuwa kutoka kwenda nje kwa ajili ya Pre Season badala yake kutumia kambi ya Avic Town kuwa sehemu ya maandalizi.
SOMA NA HII WAKATI SIMBA WAKIWA BADO ZAMBIA...LWANGA ATUA BONGO KIMYA KIMYA...AJITENGA NA WENZAKE...