Home Habari za Simba Leo COASTAL UNION WAINGILIA KATI USAJILI WA LAWI…SIMBA HAWAKUFUATA TARATIBU.

COASTAL UNION WAINGILIA KATI USAJILI WA LAWI…SIMBA HAWAKUFUATA TARATIBU.

Habari za Simba leo

NI MASAA MACHACHE tu Tangu utambulisho wa beki wa kati kutoka Coastal Union Lameck Lawi kufanyika kwenye klabu ya Simba, lakini tayari Uongozi wa wagosi wa kaya wameingilia kati usajili huo.

Kupitia kwa Afisa Habari wa Coastal Union Abbas El Sabr alisema kwamba Simba SC hawakufuata utaratibu waliopewa na Viongozi wa timu hiyo.

“Tuliwapa za kufuata kama kweli wanamtaka Lawi, lakini bahati mbaya hawakufuata taratibu tulizowapa, tukaamua kusitisha na kuwaambia hatupo tayari kufanya biashara”

Lameck Lawi (18) ni moja kati ya mabeki wa kati wa kisasa wachache sana wanaotumia mguu wa kushoto, ana uwezo pia wa kucheza beki wa kushoto, huku akimudu kucheza eneo la kiungo wa ulinzi namba 6.

Ni mchezaji mzuri mwenye kasi uwanjani, anajua kukaa kwenye nafasi kama namba 4, huku akiwa na uwezo mkubwa wa kufanya tackling na kunusa hatari kabla haijakuwa na madhara.

Makuzi yake ya soka yalianzia kwenye klabu ya KMC FC, kisha akajiunga na wagosi wa kaya kabla ya kuonwa na Simba na kisha kusajiliwa.

Soka la Bongo tuliripoti juu ya usajili huu mapema kabisa, na tunafahamu Simba walimalizana na mchezaji huyo muda mrefu wakilipa kila kitu pesa ya usajili na mshahara wa mchezaji huyo.

Lakini kuliibuka mgogoro mkubwa kwa Viongozi wa Coastal Union baada ya dili hilo, kuna baadhi yao walikubali ajiunge na Simba huku wengine wakielezwa kumtaka mchezaji huyo abakie awasaidie kwenye kombe la Shirikisho Afrika, huku wakitaja kwamba kuna timu nje ya nchi imejitokeza inamuhitaji mchezaji huo.

Usajili wa Lameck Lawi umekuja kama mbadala wa Kennedy Juma huku wakifanya mazungumzo na beki wa kati wa Asec Mimosas Antony Tra Bi Tra ili awe mrithi wa Henock Inonga.

SOMA NA HII  JEMEDARI:- CHAMA AKIZIDIWA UWEZO UWANJANI ANAFANYAGA MAMBO YA KISHAMBA SANA...