Home Habari za Simba Leo SIMBA YAMCHUKUA LAMECK LAWI…WAGOSI WA KAYA WAJIBU MAPIGO

SIMBA YAMCHUKUA LAMECK LAWI…WAGOSI WA KAYA WAJIBU MAPIGO

kennedy Juma Simba

KLABU ya Simba SC imeshakamilisha kandarasi ya beki wa kushoto wa Coastal Union Lameck Lawi, ambaye kila  kitu kipo tayari anasubiri tu kutambulishwa.

Lameck  Lawi msimu uliomalizika alikuwa na kiwango bora sana kwa WAGOSI wa Kaya, Coastal Union ambao ameisaidia timu yake kumaliza katika nafasi ya 4 ya Ligi kuu na kuifanya ishiriki kombe la shirikisho Afrika.

Simba ilifanya mazungumzo na mchezaji   huyo, na kisha kumsajili ambapo inadaiwa wamempa mkataba wa miaka miwili na mshahara mnono.

Lengo la kufanya usajili huo, Uongozi wa Simba unahitaji kutafuta mbadala na beki wao wa kushoto, Mohammed Hussein ambaye ametumika sana kwa misimu mingi, tena akiwa na kiwango bora zaidi.

Sasa basi, nao Coastal Union wamejibu mapigo kwa kuuliza uwezekano kumnasa beki wa Simba, Kennedy Juma kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja.

Kennedy Juma amekuwa mhimili mzuri wa klabu ya Simba katika safu ya ulinzi, baada ya Henock Inonga kuumia kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons,   akapona akaja kuumia tena kwenye mcheezo wa Dabi kipindi cha kwanza tu, ambapo Simba ilipoteza kwa magoli 2-1.

Inaelezwa kwamba, Inonga nae amepata timu hivyo ameuambia Uongozi wa klabu hiyo kwamba,  anahitaji kuondoka lakini Simba wamemueleza kwamba bado ana mkataba nao hovyo timu inayomhitaji awaambie waje kufanya biashara.

Kwa ufupi ni kwamba Simba inaonekana hawana mpango tena ya kuendelea na Henock Inonga kwa msimu ujao,  lakini hawataki kumuacha aondoke bure, wanahitaji kufanya biashara ya maana baada ya kitasa hicho   kuonesha kiwango kizuri sana kwenye mashindano ya AFCON huko Ivory Coast akiwa na timu yake ya Taifa ya DR Congo.

SOMA NA HII  TETESI:....MASTAA HAWA WATANO 'KULIWA VICHWA' SIMBA SC...AKPAN APATA PAKUHEMEA...