Home Habari za Simba Leo Simba Yatua kwa Kiungo Mganda…Ni Mrithi wa Thadeo Lwanga

Simba Yatua kwa Kiungo Mganda…Ni Mrithi wa Thadeo Lwanga

Kenneth Semakula

KLABU ya Simba SC Inafanya mambo  yake kimya kimya ambapo kwa sasa imeelekeza jicho lake, kwa Kiungo mkata umeme aliyekuwa anakipiga SC Villa, Jina la Kenneth Semakula ni moja ya saini inayowindwa sana na mimba hiyo ya TANZANIA ili kujiunga msimu ujao.

Uongozi wa Simba unaamini kiungo huyo wanaweza kumpata kwa gharama ndogo kwa sababu, ni mchezaji ambaye yupo huru sokoni na wanamuona ataleta tija kikosini humo baada ya kutokuwa na matumaini na Msenegali, Babacar Sarr.

Mganda huyo amekuwa  na kiwango bora sana kwa msimu uliomalizika, akiwa ameisaidia timu yake kutwaa ubingwa wa Ligi hiyo na kuifanya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2024/25

Kwa hapa Tanzania Kenneth Semakula amekuwa akihitajika na vila viwili, Azam FC na Simba SC, ambapo kila mmoja amekuwa akifanya nae mazungumzo, lakini hadi sasa Mnyama anapewa nafasi kubwa ya kuinasa saini ya kiungo huyo.

Simba inataka kuona kama wanaweza kupata bahati kama waliyoipata kwa Thadeo Lwanga ambaye ni Mganda aliyefanya vizuri sana klabuni hapo.

Kwa upande wa Yanga wana wachezaji wa Kiganda, huku nafasi ya Khaled Aucho ikiwa haina mpinzani, japokuwa watu wengine wana hofu na uwezo wa Ligi ya Uganda kwamba ndi mdogo kulinganisha na wa Tanzania, hivyo wachezaji wengi wanaotoka Ligi hizo huwa wanashindwa kuonesha uwezo wao kiushindani.

SOMA NA HII  PICHA YA FEITOTO INAYOTREND MTANDAONI...YANGA YAONYWA