Home Habari za Yanga Leo PICHA YA FEITOTO INAYOTREND MTANDAONI…YANGA YAONYWA

PICHA YA FEITOTO INAYOTREND MTANDAONI…YANGA YAONYWA

feitoto

BAADA ya  Klabu ya Yanga kutwaa taji lao la 3 mfululizo,  Kombe la Shirikisho la CRDB waliposti picha kwenye Ukurasa wao wa Klabu upande Instagram, picha hiyo inamuonesha mchezaji  wao wa zamani Feisal Salum Feitoto kwa mbali akiwa hana  furaha.

Picha hiyo ilisindikwa na Ujumbe uliosemeka “KAMA NANENO NI MKUKI” sijui Yanga walikuwa na maana gani,  au labda ni utani wa mpira tu ndicho walikuwa wana maanisha kwa mchezaji wao wa zamani, anayekipiga Azam FC.

Feitoto alikuwa a kiwango bora sana kwenye mchezo huo wa fainali, alipokuwa akienda kupiga penati mashabiki wa Yanga walikuwa wakimzomea, lakini alipiga na kufunga ile penati ndipo alipowageukiwa na kuwafunga midomo.

Picha hiyo imezua gumza kubwa, na kila mtu ameipokea kwa maana yake  huko mitandaoni,  lakini baadhi ya wachambuzi na waandishi wa habari, wadau wa Sok akiwemo Wilson Oruma aliandika hiki kwenda kwa Yanga.

“Kwa bahati mbaya sana hata aliyeposti anaweza asielewe naongelea Kitu Gani hapa”.

“Mtu mmoja anaweza Kusema mbona yeye FEISAL SALUM alitunyamazisha wakati alipofunga Penalty?

“Kwa mchezaji unaweza ukamuelewa Kwasababu alikuwa anazomewa sana wakati anaenda Kupiga ule Mkwaju wa Penalty”.

“Sisi huku tunachanganya ushabiki na a really Professional Life. Hii Picha Ingeweza kwenda kwenye page za udaku huko na Mashabiki”

“Lakini sio ya Kupostiwa kwenye page rasmi ya club na Kuandika caption za Kidaku ” Kama meneno Mkuki” Wilson Oruma- Mzee wa Jambia.

Pia Feitoto hakuonekana kabisa kwenye zoezi la kuvishwa medali za mshindi wa pili, hii bila shaka ni kutokana na uchungu wa kupoteza fainali aliokuwa nao kiungo huyo.

SOMA NA HII  KINDA LA YANGA MAMBO FRESH UGANDA