Home Habari za Yanga Leo KIFAA ALICHOPATIWA DIARRA CHAWAPA YANGA UBINGWA.. UBINGWA MARA 4 MFULULIZO.

KIFAA ALICHOPATIWA DIARRA CHAWAPA YANGA UBINGWA.. UBINGWA MARA 4 MFULULIZO.

Yanga Bingwa

Mechi ya kisasi imeisha kwa Yanga kutwaa ubingwa wa 4 mfululizo, baada ya kuwafunga Azam FC kwa mikwaju ya penati 5-6, huku mlinda mlango wa klabu hiyo Djigui Diarra akiibuka shujaa baada ya kupangua mikwaju ya penati 2.

 

Siku ilitaka kuwa mbaya kwa Yanga ambao walianza kwa kukosa mikwaju miwili ya penati, Aziz Ki na Joseph Guede walikosa penati za mwanzoni, lakini Diarra aliwarudisha mchezoni.

Makocha wa timu zote mbili walizingumzia mchezo wenyewe huku Gamondi akitoa pongezi zaidi kwa wachezaji wake.

“Leo tulikuwa vizuri, kipindi cha kwanza timu ilitengeneza nafasi lakini hatukuweza kuzitumia, kipindi cha pili Azam FC walijaribu kuwa nyuma na kipa wao kupoteza muda lakini tumeshinda kwa mikwaju ya penati”

“Kwa wachezaji na benchi la UFUNDI tunatakiwa kuamini hadi mwisho wa mchezo, haijalishi tulikosa penati mbili lakini tulikuwa tunaamini tunaweza kuchukua ubingwa” Muguel Gamondi.

Kwa upande wa kocha msaidizi wa Azam FC, Yusuf Dabo alielezea hisia zake baada ya kupoteza ubingwa huo ambao ungekuwa wa pili kwao tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo mwaka 1967.

“Wapinzani walipoteza mikwaju miwili, na sisi hatukuweza kuzitumia hizi nafasi kumaliza mchezo, niwapongeze wachezaji leo tulikuwa bora lakini tumekuja kupoteza kwenye penati, hazina mwenyewe” Kocha Msaidizi wa Azam FC Yusuf Dabo.

Mchezaji bora wa mashindano hayo alikuwa ni Ibrahim Bacca, ambapo alisema haya baada ya mchezo kumalizika.

” Ilikuwa ni mechi nzuri, lakini kwa uimara wetu na ubora wetu tumeweza kutetea ubingwa huu” Ibrahim Bacca Mchezaji bira wa mchezo.

“Tuliweza kupambana dakika 120 lakini tulienda kwenye mikwaju ya penati ambayo haina mwenyewe, na Yanga wamechukua”

“Kwa siku kama ya leo kipa alicheza penati mbili lakini timu tukashindwa kutumia nafasi, nimpe polee kipa wetu (Mustafa Mohamed) kwa kukosa kombe” Lusajo Mwaikenda.

Kwa upande wa Rais wa Yanga Eng Hersi Said alisema kwamba, licha ya kuwa na msimu bora lakini watasajili ili kuongeza ubora zaidi kwenye kikosi chao.

“Haikuwa rahisi, mchezo ulikuwa mzuri na hadhi ya fainali, nimpongeze Gamondi, lakini mwaka huu hatukuwa bora sana kwenye mikwaju ya Penati, tulipoteza dhidi ya Simba, na Mamelodi na leo na Azam FC, mashabiki na wanachama wameona ila niwapongeze wachezaji na benchi la ufundi kwa ubingwa huu” Rais wa Yanga Eng Hersi Saidi.

“Tunaendelea kujenga timu imara, na kusafanya sajili nzuri kuendelea kuimarisha timu yetu ili iwe na ushindani mkubwa zaidi” Eng Hersi Saidi

SOMA NA HII  TATIZO WABONGO TUNADHARAU SOKA LETU...SIMBA NA YANGA NI TISHIO KUBWA CAF