Home Habari za Yanga Leo FAINALI YA FA AZAM FC VS YANGA, KIPINDI CHA KWANZA…YANGA ANASHAMBULIA SANA

FAINALI YA FA AZAM FC VS YANGA, KIPINDI CHA KWANZA…YANGA ANASHAMBULIA SANA

Yanga sc

Mechi dume, unaweza kusema ni fainali bora kwa dakika 45, za kwanza zimetamatika bila kwa ubao kusoma 0-0, si Azam FC wala si Yanga SC ambae amefanikiwa kuliona lango mwenzake.

 

Dakika 25 Clement Mzize alikosa goli akiwa kwenye nafasi nzuri kabisa lakini, mlinda mlango wa Azam FC Mohamed alikuwa shujaa na kuikoa timu yake.

Dakika ya 27 tena Clement Mzize alimtengenezea mpira mzuri Stephen Aziz Ki nje ya 18, akafinya na kuukata mpira ulioenda moja kwa moja hadi lango, lakini bado Mohamed akachomoa shuti hilo kwa mkono wake wa kushoto, ambalo huenda lingepigilia msumari wa moto.

Kwa ujumla kipindi cha kwanza kilikuwa cha kasi sana, huku matukio kadhaa yakijitokeza, ambapo dakika ya 30 Yanga walipata faulo iliyopigwa na Aziz Ki lakini mlinda mlango wa Azam akaokoa mchomo huo, Whaat a save kutoka kwa Mustafa Mohamed yeye ndiye Man Of the Match kwa Azam FC.

Timu zote mbili zilikuwa zinashambiliana kwa kupokezana, huku Azam FC wakitawala zaidi dakika 20 za kwanza kwa majaribio kadhaa waliyoyafanya lakini, safu ya ulinzi ya Yanga SC ilikuwa bora na kuonesha ni kiasi gani wana uzoefu wa kucheza fainali.

KIKOSI CHA YANGA KILICHOANZA

1. Djigui Diarra

2. Yao Athohola Kwasi

3. Joyce Lomalisa

4. Ibrahim Bacca

5. Dickson Job

6. Khaled Aucho

7. Maxi Nzengeli

8. Paccome Zouazoa

9. MUDATHIR Yahya

10. Aziz Ki

11. Clement Mzize

KILICHOANZA CHA AZAM FC

1. Mustafa Mohamed

2. Lusajo Mwaikenda

3. Paschal Msindo

4. Fuentes

5. Yannick Bangala

6. Yahya Zaidi

7. Adolf Mtasingwa

8. Kipre Jr

9. Abdul Suleiman Sopu

10. Feisal Salum, Feitoto

11. Gibril Sillah

SOMA NA HII  SIMBA WALIVYOPIGWA KO NA YANGA USAJILI WA AZIZ KI...ISHU NZIMA HII HAPA A-Z