Home Habari za Yanga Leo YANGA YAMPATIA DIARRA KIFAA MAALUM..KINAZUIA MAGOLI… NAMNA KINAVYOFANYA KAZI

YANGA YAMPATIA DIARRA KIFAA MAALUM..KINAZUIA MAGOLI… NAMNA KINAVYOFANYA KAZI

KATIKA kuelekea mchezo wa fainal ya kiume, vita ya kisasi kwa Azam FC mbele ya Yanga, mabosi wa Yanga wameshtukia mchezo mapema, na kuamkua kuwatafutia walinda mlango wao vifaa maalum vya kuzuia mabao.

Yanga ni kama wapo ulaya tu, wanafanya mambo kisasa sana hawa jamaa, na ukitaka kujua hilo hivi karibuni walitambulisha kifaa cha kupiga mipira kwa walinda mlango “ ball launcher

Hiyo haikutosha juzi tu katika mazoezi yao wamezindua kifaa kingine maalum kwa kuimarisha uwezo wa makipa wao akiwemo nyanda namba moja Djigui Diarra.

Yanga wanawajua vizuri Azam FC, msimu huu wamekuwa na moto sana, kuna Abdul Suleiman Sop kiboko ya Diarra, na Feitoto aliyepigili msumari wa moto kwenye mzunguko wa pili pale wa Mkapa.

Yanga katika kujiandaa na mchezo huo chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, alikitambulisha kifaa hicho katika siku ya pili ya mazoezi.

Kifaa hicho cha kisasa ni miwani ambayo kitaalamu inaitwa “Strobe Eyewear au Strobe Glasses” na Kocha wa Makipa wa Yanga, Alaa El Meskini, alikuwa akiwanoa Diarra, Aboutwalib Mshery na Kassim, huku wakiwa wamevaa kifaa hicho machoni, huku wakipigiwa mipira na kudaka kwa ufasaha.

JINSI KINAVYOFANYA KAZI

Kifaa hiki kimetengenezwa maalum kwa ajili ya kumfanya mtumiaji kufanya uamuzi wa haraka na sahihi kwani macho yanapoona basi taarifa hufika kwa haraka zaidi kwenye ubongo.

Unapovaa kifaa hicho, uchakataji wako wa taarifa unakuwa wa haraka zaidi jambo linalofanya utendaji wako wa kazi kuwa wa kasi na fasaha.

Kipa akivaa kifaa hicho humfanya kudaka michomo mingi kwa usahihi na nadra sana kuruhusu kufungwa kwani macho yake yanapouona mpira, taarifa inafika kwa haraka kwenye ubongo na kurudisha majibu kwa kasi inayomfanya kuwa tayari kufanya uamuzi sahihi.

Thamani ya kifaa hicho inakadiriwa ni Dola 299 (Sh774,506).

FAIDA ZA KIFAA HIKI

Kuongeza umakini, hii inayafanya macho yako kuwa kwenye tukio jambo linalokufanya uende sawasawa na hali ya mchezo.

Ukitumia kifaa hiki, pia huyawezesha macho yako kuona vizuri zaidi ya ilivyo kawaida, pia hukufanya kuwa mwepesi katika kufanya maamuzi sahihi.

Pia kuufanya mwili wako kuwa kwenye sehemu sahihi ya kufanya uamuzi kwani kinakupa uwezo wa kuona pembeni na mbele yako kuna hatari gani.

SOMA NA HII  YANGA YATUA KA MKATA UMEME...ANATOKA DR CONGO