Home Habari za Yanga Leo SABABU 4…KWANINI FAINALI YA LEO…NI VITA YA KISASI?

SABABU 4…KWANINI FAINALI YA LEO…NI VITA YA KISASI?

HABARI ZA YANGA

WATU wengi wanasema na wengine kusikia tu hii ni fainali ya kisasi kwa timu zote mbili Yanga SC na Azam FC, lakini hawajui sababu ni nini Soka La Bongo tunakusogezea sababu kuu 4 ni kwanini fainali ya leo ya FA ni sawa na Vita ya kisasi?

Hii ni fainali ya tisa tangu kurejeshwa kwa michuano ya FA iliyoanzishwa 1967 ikifahamika kama Kombe la FAT kisha kuwa Kombe la FA na kuzimika 2002, kala ya kufufuka tena 2003.

FAINALI YA WABABE WA LIGI KUU

Ni bonge la fainali inayozikutanisha timu zilizomaliza nafasi mbili za juu za Ligi Kuu Bara hivi karibuni, huku zote zilikuwa zikichuana vikali na kupokezana kiti cha uongozi kabla ya watetezi Yanga kufanya yao na kutetea ubingwa kwa msimu wa tatu mfululizo na Azam kushika nafasi ya pili.

VITA YA UFUNGAJI BORA IMEHAMIA HUKU

Fainali hii inawakutanisha wachezaji waliokuwa na vita ya kuwania kiatu cha Mfungaji Bora wa Ligi, Stephane Aziz KI na Feisal Salum ‘Fei Toto’ lakini mbabe alikuwa MBUKINABE akifunga mabao 21 dhidi ya 19 ya Fei.

Na leo tena kuna vita nyingine ya nyota wa timu hizo wanaowania ufungaji bora wa Shirikisho kati ya Clement Mzize mwenye mabao matano na Abdul Suleiman ‘Sopu’ mwenye mabao manne.

KISASI HA KUPOTEZA

Kubwa zaidi ni mechi ya kisasi kwa timu zote. Ndio, katika pambano la mwisho kwa timu hizo kukutana katika Ligi Kuu Bara, Yanga ilicharazwa mabao 2-1, hivyo leo itataka kulipa kisasi cha kipigo hicho.

Lakini kwa Azam inataka kulipa kisasi cha kufungwa katika fainali mbili ilizokutana na Yanga kwenye Kombe la Shirikisho, ikianza kwa kunyukwa mabao 3-1 msimu wa 2015-2016 kisha kulala 1-0 msimu uliopita jijini Tanga na iwapo leo haitakomaa itakuwa inapigwa fainali ya tatu na wababe hao wa nchi.

KILA TIMU INATAKA KOMBE

Yanga itaingia uwanjani ikiwa na shauku kubwa ya kutetea ubingwa wake, wakati Azam inahitaji kulipa kisasi cha msimu uliopita baada ya kupoteza fainali mbele ya Yanga kwa bao 1-0. Azam imekuwa ni mchekea tu mbele ya Yanga kila walipokutana katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo.

Msimu wa 2015-2016 wakati michuano hiyo iliporejea kwa mara nyingine, Yanga iliifunga Azam mabao 3-1, wafungaji wakiwa ni Deus Kaseke na Amissi Tambwe alifunga mabao 2, bao la Azam mfungaji alikuwa Didier Kavumbagu.

Msimu uliopita timu hizo zilikutana tena fainali kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Yanga ikashinda 1-0 kupitia Kennedy Musonda.

Safari hii Azam FC inaonekana haitaki utani, italipa kisasi huku pia hesabu zake zikiwa ni kumaliza msimu angalau na taji moja.

SOMA NA HII  KISA YANGA KUPONGEZWA NA MO DEWJI....KAMWE AIBUKA NA HILI JIPYA...'AMNYEA' AHMED ALLY ..