Home Habari za usajili Simba leo FEITOTO YUKO TAYARI KWENDA SIMBA…ANAWASIKILIZA VIONGOZI

FEITOTO YUKO TAYARI KWENDA SIMBA…ANAWASIKILIZA VIONGOZI

feitoto

KIUNGO mshambuliaji wa Azam FC, Feisal Salum Feitoto, amesema haoni shida yoyote kujiunga na klabu ya Simba SC kama itamhitaji, ila inachotakiwa ni kufuata taratibu zote za uhamisho, kwani bado ana mkataba.

Feitoto ambaye kipindi hiki cha usajili anahusishwa na Simba SC, amesema hana tabu na yupo tayari kujiunga na timu hiyo kwa msimu ujao wa Mashindano.

Kwa mujibu wa Spotileo, Feitoto amejibu tetesi za yeye kwenda Simba na kubainisha kwamba, kwa upande wake haoni tabu kukipiga mitaa ya Msimbazi, muhimu taratibu za usajili zifuatwe tu.

“Nipo tayari kucheza Simba na nitacheza kwa moyo mmoja, mpira ni kazi yangu na nitacheza timu yoyote, hilo la thamani ya mkataba hilo lipo kwa uongozi wa timu yangu,” amesema Kiungo huyo wa Azam FC.

Ofisa habari wa Azam FC, Hashim Ibwe amesema hawajatangaza kumuuza Feitoto, lakini kuna klabu au timu ikimuhitaji analazimika kuvunja mkataba kwa kipindi kilichobakiwa wenye thamani ya dola za kimarekani Million 2.

“Hatujawahi kuwa wachoyo na mtu ambaye ana muhitaji mchezaji hapa Azam FC, kwa sababu tumekuwa na wachezaji na kuwaacha na kwenda katika klabu mbalimbali akiwemo Aishi (Manula), Kapombe (Shomari), Erasto (Nyoni), Mudathir (Yahya) na Salum Aboubakar.

“Hatujatangaza ofa juu ya Fei Toto bali kama kuna klabu au timu ambayo inamuhitaji kiungo huyo tunawakaribisha waje mezani, timu imefanya thamani ya mkataba wa mchezaji huyo na kuona sawa na kiasi hicho,” amesema Hasheem Ibwe.

Hivi karibuni Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema wapo tayari kuvunja benki kutoa kiasi cha thamani ya mkataba wa kiungo huyo wa Azam FC kwa msimu ujao.

Amesema Simba inayohitaji mchezaji hawawezi kushindwa ni suala la muda tu kwa sabau ya wanalazimika kuvunja bank , kutoa kiasi cha fedha ambazo watamnunua kutoka Azam FC, makubaliano ya pande zote kulingana na maslahi.

“Ni kweli hao mchezaji huyo yupo kwenye mipango yetu suala la kuweka fedha mazeni na kumchukuwa, kuna wachezaji wengine wapya tunawafatilia sokoni kulingana na mapendekezo ya benchi la ufundi, kwa ajili ya kuwasajili na kuimarisha kikosi cha timu yetu kwa msimu ujao,” amesema Ahmed.

SOMA NA HII  SIMBA KUVUTA 'MDAKA MISHALE' WAO KUTOKA BURUNDI....JAMAA ANADAKA MPAKA HEWA...