Home Habari za usajili Simba leo USAJILI WA KAPUMBU SIMBA…AHEMD ALLY ATOA KAULI

USAJILI WA KAPUMBU SIMBA…AHEMD ALLY ATOA KAULI

Habari za usajili Simba

KLABU ya Simba imekamilisha dili la kiungo wa Zesco United ya Zambia,  Kelvin Kapumbu kutua ndani ya kikosi cha wekundu wa Msimbazi hao kwa msimu uajo.

Imeelezwa kuwa watu maalum walipewa jukumu ya usajili wapo nchini Zambia kwa ajili ya kukamilisha dili la kiungo huyo kutua Msimbazi kuongoza nguvu ndani ya timu hiyo.

Taarifa zilizopatikana jana kuwa, kila kitu kimeenda vizuri kwa mchezaji huyo na uongozi wa Simba na makubaliano ya miaka miwili.

“Kapumbu msimu ujao ni nyekundu na nyeupe baada ya dili lake na Simba limeenda vizuri ,  usajili huo ni kulingana na mapendekezo ya benchi la ufundi baada mapungufu ya timu,” alisema mtoa habari huyo.

Kwa mujibu wa Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano,  Ahmed Ally kuwa kuanzia msimu ujao utakuwa wa furaha kwa sababu tajiri ameingia kazini.

“Agosti mwaka huu tutakuwa na furaha sana kwa sababu usajili unaofanywa mkubwa, niwaombe wanasimba watulie mambo mazuri yanakuja, ” amesema Ahmed.

SOMA NA HII  AHMED AWATOA HOFU SIMBA...HATUOGOPI YEYOTE CAF