Home Habari za Simba Leo KIMEELEWEKA HUKO…MRITHI WA BENCHIKA SIMBA AMEPATIKANA

KIMEELEWEKA HUKO…MRITHI WA BENCHIKA SIMBA AMEPATIKANA

HABARI ZA SIMBA-STEVE KOMPHELA
Steve Komphela, coach of Mamelodi Sundowns reacts during the DStv Premiership 2020/21 match between Mamelodi Sundowns and Golden Arrows at Loftus Versfeld, Pretoria, on 28 April 2021 ©Samuel Shivambu/BackpagePix

BAADA ya kupitia wasifu wa makocha mbalimbali, uongozi wa Simba umejiridhisha na uwezo wa Steve Komphela , raia wa Afrika kusini kuja kurithi mikoba ya Abdelhak Benchikha.

Inaelezwa kwamba Steve Komphela ambaye kwa sasa anafundisha klabu ya  Golden Arrows inayoshiriki Ligi kuu ya Afrika Kusini, anatajwa kuwa ndiye anaweza kuwa mrithi wa nafasi ya Benchika ambayo ilikuwa ikikaimiwa na Juma Mgunda.

Mtoa habari huyo alisema Simba wameingia makubaliano na kocha huyo , kuja kukinoa kikosi cha Simba kwa msimu ujaokwani wamedhamilia kuja kivingine.

“Suala la kocha sasa limeshafungwa tayari tumemalizana na Steve na anakuja kuchukuwa nafasi ya Benchika,  atakuwepo na timu ikienda ‘pre season’,” amesema mtoa habari huyo.

Aliongeza kuwa hata suala la usajili amekuwa akishirikiana na watu waliopewa jukumu hilo kulingana na jinsi mapungufu ya timu hiyo alivyoona katika michezo mbalimbali.

Wasifu wa Kocha huyu ambaye amefundisha kama kocha mkuu wa Mamelodi na kocha msaidizi chini ya makocha wakubwa kama Pitso (Mosimane) na Mokwena (Rhulani) , nadhani imewavutia zaidi Simba hadi kufikia hatua ya kumtaka haraka.

Ni muumini wa mfumo wa 4-4-2 , amefundisha kama kocha Mkuu Golden Arrows, 2023/24 (Julai4- Feb 19-2024), Moroka Swallows, Oktoba 24, 2022/23: Mamelodi Sundowns,  (Kocha Msaidizi), 2020/21, Mamelodi  Sundowns, Kocha Mkuu.

Kocha huyo, kwa wakati tofati amewahi kuwa kocha Mkuu wa vilabu kama, FS Stars, Platnum Stars, Afrika ya Kusini chini ya umri wa miaka 20, Dynamos FC na Maning Rangers.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally aamesema uongozi haujampa taarifa kamili na anatambua mchakato wa utafutaji kocha unaendelea.

“Mchakato wa kutafuta kocha unaendelea na upo chini ya Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Simba,  Mohammed Dewji na timu yake maalum  tunatarajia kupata mwalimu mwenye vigezo,” anasema  Ahmed.

SOMA NA HII  SIMBA HARAKA WAANZA KUTAFUTA STRAIKA LA MABAO