Home Habari za Simba Leo KOCHA MPYA SIMBA STEVE KOMPHELA…APEWA MAMBO 3 YA KUANZA NAYO

KOCHA MPYA SIMBA STEVE KOMPHELA…APEWA MAMBO 3 YA KUANZA NAYO

steve komphela- Habari za Simba leo

Kama ulivyoripoti wiki hii ni kwamba Simba ipo kwenye mazungumzo ya mwisho na Kocha Steve Komphela (56) kutoka Afrika Kusini ili kurithi mikoba ya Abdelhack Benchikha siku chache kabla ya msimu kumalizika.

Kama kila kitu kitaenda sawa Steve Komphela atatambulishwa kuwa kocha mkuu wa Simba kwa msimu ujao wa 2024/2025, licha ya kwamba anapingwa na baadhi ya viongozi wa juu wa timu lakini anaonekana kuwa na nafasi kubwa.

Komphela ni mzoefu wa soka la Afrika kwani amefundisha timu mbalimbali tangu mwaka 2002, lakini kubwa zaidi ni Kaizer Chiefs, Mamelodi Sundowns na timu ya taifa ya Afrika Kusini Bafana Bafana.

MAMBAO HAYA ATATAKIWA KUANZA NAYO

KUTENGENEZA TIMU YA USHINDANI

Kama Steve Komphela ataajiriwa Simba au kocha mwingine, moja kazi atakayokuwa nayo kwenye kikosi hicho ni kutengeneza timu mpya kabisa.

Hii ina maana sehemu kubwa ya wachezaji wa Simba wataondoka baada ya baadhi kumaliza mikataba, lakini wengine wataachwa na kuuzwa, kutokana na wachezaji wengi msimu uliopita kuonekana kuwa chini ya kiwango hali ilyochangia timu hiyo ikose matokeo mazuri kwenye mechi zake.

Uongozi wa timu hiyo tayari umeshasema kuwa kuna wachezaji wataondoka kwenye timu hiyo na hivi karibuni itawatangaza pia kusajili wapya.

Hapo kocha mkuu atakuwa na kazi ya kuijenga timu hiyo upya bila kujali wachezaji atakaowasajili yeye ama atakaowakuta.

KUTULIZA PRESHA YA MASHABIKI

Kila Mwanasimba anatamani kuiona timu hiyo inatwaa makombe msimu ujao baada ya kuyakosa kwa misimu mitatu mfululizo. Hiyo tayari ni presha kwa kocha mpya atakayetambulishwa Simba kwa kuwa mashabiki hawawezi kuvumilia kukosa ubingwa msimu wa nne mfululizo.

Kocha mpya ana kazi ya kurejesha furaha na kupunguza presha kwa wadau, wanachama na mashabiki wa timu hiyo ambao wamechoka kushuhudia watani wao Yanga wakitwaa makombe kila msimu, lakini wakiwa wanataka kuona timu hiyo inatimiza malengo kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika angalau kufika nusu fainali.

HESHIMA YA DABI

Jambo lingine ni Dabi ya Kariakoo. Mechi yenye mvuto na msisimko wa hali ya juu.

Kocha mpya wa Simba anakuja wakati timu hiyo ikiwa na kidonda kikubwa kutoka kwenye dabi. Imepoteza mechi mbili zote za ligi kwa msimu uliopita mbele ya mtani wake, Yanga na kubwa zaidi ilichapwa idadi kubwa ya mabao kwa jumla ya 7-2 kwenye mechi mbili za ligi.

Kocha atakutana na presha hii na kwa bahati mbaya mechi yake ya kwanza ya mashindano itakuwa dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii. Akishinda ataanza kurudisha imani kwa mashabiki wa timu hiyo bila kujali timu imechezaje.

SOMA NA HII  SIMBA YAANZA KIJIANDAA MAPEMA CAF...WAPINZANI MTEGONI