Home Habari za Simba Leo SIMBA YAANZA KIJIANDAA MAPEMA CAF…WAPINZANI MTEGONI

SIMBA YAANZA KIJIANDAA MAPEMA CAF…WAPINZANI MTEGONI

HABARI ZA SIMBA

MNYAMA Simba ameanza mambo yake mapema ya kuwafuatilia wapinzani wake katika hatua ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo kwa asilimia kubwa wanakwenda kucheza dhidi ya Al Ahli Tripoli ya Libya ambao tayari mchezo wa kwanza wameifunga Uhamiaji mabao 2-0.

Katika kuhakikisha Simba inafuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo, imepanga kumtuma mtu wao maalum wa kwenda Libya kuwasoma vilivyo Al Ahli Tripoli katika mchezo wao wa marudiano dhidi ya Uhamiaji utakaochezwa Jumamosi ya wiki hii kwenye Uwanja wa Tripoli nchini humo.

“Mipango ya kufanya vizuri michuano ya kimataifa inaendelea na wiki hii kuna mtu wetu ataenda Libya kwa ajili ya kushuhudia mchezo wa marudiano kati ya Al Ahli Tripoli dhidi ya Uhamiaji.

“Tunataka kuwafahamu vizuri wapinzani wetu namna mbinu zao zilivyo ili kupata mwanga wa nini tunapaswa kwenda kukifanya tukielekea kucheza nao,” kilisema chanzo.

Simba itacheza dhidi ya mshindi kati ya Al Ahli Tripoli na Uhamiaji katika hatua ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika kuwania kufuzu makundi ambapo timu hiyo malengo yao msimu huu ni kuona wanafika hadi fainali.

SOMA NA HII  KAMBI YA YANGA IMENOGA...AUCHO NA DIARRA WAONGEZA MZUKA