Home Habari za Simba Leo SIMBA KUSHUKA DIMBANI LEO…KUFUZU CAF

SIMBA KUSHUKA DIMBANI LEO…KUFUZU CAF

HABARI ZA sIMBA

Timu ya wanawake kutoka Tanzania Simba Queens, inatarajiwa kushuka dimbani leo dhidi ya Kawempe Muslim FC kutoka nchini Uganda katika Uwanja wa Abebe Bekila, leo Agosti 21, 2024 majira ya saa 5:00 asubuhi, ikiwa ni mchezo wa mashindano ya CECAFA Zonal Qualifiers kwa ajili ya CAF Women’s Champions League.

Ikumbukwe kuwa mchezo wa kwanza wa klabu ya Simba Queens walipata ushindi wa goli 5-0 dhidi ya FAD Djibouti.

Mara ya mwisho Simba Queens ilifika hadi hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mabingwa la Africa na kuondoshwa na Mamelod Sundowns ya Afrika kusini.

SOMA NA HII  MAMA SAMIA AMWAGA MANOTI TAIFA STARS...MASTAA WAPAGAWA