Home Uncategorized YANGA: TUNAIFUNGA SIMBA MACHI 8 MAPEMA TU

YANGA: TUNAIFUNGA SIMBA MACHI 8 MAPEMA TU


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa umejipanga kuona unapata matokeo chanya kwenye mechi zake zote za Ligi Kuu Bara ikiwa ni pamoja na mchezo wa watani wao wa jadi Simba utakopigwa Machi 8 Uwanja wa Taifa.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa baada ya kumaliza gundu la sare sasa hesabu zao ni kuona wanashinda mbele ya Simba Machi 8.

“Tumewachapa Alliance licha ya manenomaneno, kwa sasa tupo tayari na hata mchezo wetu wa mwezi Machi tutawashinda wapinzani wetu, wape salaamu,”.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa Simba ikiwa mwenyeji ililazimisha sare ya kufungana mabao 2-2

SOMA NA HII  VIDEO: HAYA NDIYO ALIYOSEMA MZEE KILOMONI BAADA YA KUACHIWA NA POLISI