Home Habari za Simba Leo ORLANDO PIRATES WAPIGWA KO NA SIMBA…MCHEZAJI WAMEPITA NAE

ORLANDO PIRATES WAPIGWA KO NA SIMBA…MCHEZAJI WAMEPITA NAE

HABARI ZA USAJILI SIMBA

Klabu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini inadaiwa kumshawishi kiungo Augustine Okejepha ajiunge nao akitokea klabu ya Rivers United ya Nigeria.

Hata hivyo Pirates wameambulia patupu baada ya mchezaji huyo kuweka msimamo kuwa msimu ujao atacheza klabu ya Simba ya Tanzania.

Taarifa za uhakika ni kuwa Simba ilikamilisha usajili wake mapema mwezi huu, na kinachosubiriwa ni utambulisho wake ambao umepangwa kufanywa muda wowote kuanzia sasa.

Imeelezwa Pirates walikuwa tayari kutoa Milioni 500 kwa ajili ya kumsajili mchezaji huyo bora wa kikosi cha Rivers United msimu uliopita.

Okejepha anatarajiwa kuwasili nchini wiki ijayo sambamba na wachezaji wengine waliosajiliwa na Simba tayari kwa pre-season itakayofanyika huko Misri.

Wachezaji wa Simba wanatakiwa kuanza kuripoti Dar kuanzia Julai 1, ili kufanya mazungumzo kabla ya timu hiyo kwenda kuanza maandalizi ya msimu huko Misri.

Afisa Habari wa Simba Ahmed Ally akizungumzia usajili wa timu hiyo amesema kwamba, usajili wao umekamilika kwa asilimia 97%

“Usajili wetu umekamilika kwa 97%, hivyo muda wowote tunaanza kutambulisha vyuma vipya, kuna huyo mchezaji tumemsajili ni mrefu zaidi ya goli, haruki anafunga tu”

“Kuna mchezaji mwingine anatoka DR Congo, na kuna huyo mmoja anakimbia kama treni mpya SGR” Alisema Ahmed Ally.

Kuhusu wachezaji ambao wanaachwa na klabu hiyo Semaji alisema kwamba hadi sasa wamefikia kama kiasi cha asilimia 45 tu kati ya wote wanaohitajika kuachwa.

SOMA NA HII  BODI YA LIGI YAIJIBU SIMBA KUHUSU UWANJA.