Home Habari za Simba Leo BODI YA LIGI YAIJIBU SIMBA KUHUSU UWANJA.

BODI YA LIGI YAIJIBU SIMBA KUHUSU UWANJA.

HABARI ZA SIMBA NA YANGA

BODI ya Ligi imeweka wazi kwamba kuna maboresho kwenye Kanuni za ligi msimu wa 2024-25 ambapo zinaruhusu timu za Ligi kuu ikiwemo Simba na Yanga kutumia viwanja vya Unguja na Pemba visiwani Zanzibar ikiwa vitakidhi vigezo.

Almas Kasongo alisema kuwa baadhi ya kanuni za ligi msimu ujao wa 2024/25 ni kuwa uwanja ambao hautakuwa na viti elfu tatu (3,000) kwa ajili ya mashabiki havitatumika kwenye michezo ya Ligi Kuu.

“Jana nimepokea barua ya timu ya Ligi Kuu kutumia uwanja wa Zanzibar kama uwanja wao wa nyumbani. Timu yeyote ya Tanzania Bara, ikiamua kutumia uwanja wowote visiwani (Unguja/Pemba) ruksa,” alisema Kasongo.

Itakumbukwa kuwa, msimu uliopita Simba iliandika barua kwa Bodi ya Ligi kuomba uwanja wa Amaan kuwa uwanja wao wa nyumbani, lakini kulingana na kanuni za ligi zilizokuwepo, Simba haikuruhusiwa kutumia uwanja huo.

Lakini kukamilika kwa uwanja wa KMC FC Mwenge unaipa nafasi Simba kuchagua watumie uwanja huo, au wapeleke mechi zao Unguja.

Hiyo itakuwa faidi kwa mashabiki wa Zanzibar kuona timu yao, na Simba itapata mapato, lakini suala ni moja tu endapo muitiko utakuwa mdogo wa mashabiki.

SOMA NA HII  KUWANIA LIGI YA MABINGWA AFRIKA KWA WANAWAKE...SIMBA QUEENS WAIZIDI KUTIKISA AFRIKA...