Home Habari za Simba Leo BODI YA LIGI YATOA TAMKO…AHMED ALLY NA WENZAKE KUACHA UCOMEDY

BODI YA LIGI YATOA TAMKO…AHMED ALLY NA WENZAKE KUACHA UCOMEDY

Habari za Yanga leo

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB), Almas Kasongo amesema msimu watatoa adhabu kwa Maofisa Habari wa timu wanaochekesha na kushindwa kuzungumzia Mpira huku akizikumbusha klabu kufuata kanuni kwa kuajiri maafisa habari wenye elimu ya habari.

“Kuna Muda unamsikiliza Ofisa Habari wa timu na kujiuliza, huyu ni kiongozi wa timu au mchekeshaji? Niseme tu ndugu zangu, msimu ujao 24|25 tutadili na watu hawa kwa kuwapa adhabu,“ amesema Almas Kasongo.

Miongoni mwa Maafisa Habari wanye mvuto kwa sasa mitandaoni ni Ahmed Ally wa Simba, ambaye ameibuka kuwa kipenzi cha mashabiki kwa kumuigilizia sauti na clips zake za mahojiano.

Moja ya Clip ya Video inayosambaa sana mitandaoni kwa sasa ni ile ambayo anawaita waandishi wa Habari waje kufanya nae mahojiano, baada ya mechi ya Simba Day kuisha.

Kwa sasa Haji Manara nae amerudi kundini ikiwemo wenzake Ali Kamwe na Privadinho akiwemo Abdulaaziz.

SOMA NA HII  LIGI YA MABINGWA AFRIKA...SIMBA WAPELEKWA MALAWI...YANGA WAPEWA WASUDANI KUSIN...MECHO ZOTE KUPIWA HIVI...