Home Habari za Yanga Leo PACOME KUELEKEA DABI ATOA KAULI HII YA KIBABE

PACOME KUELEKEA DABI ATOA KAULI HII YA KIBABE

Habari za Yanga leo

Kuelekea katika mechi ya dabi itakayochezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa, kiungo wa Yanga Pacome Zouzoua amefunguka kuhusu mwanzo wake mpya.

Kocha wa kikosi hicho, Miguel Gamondi aliweka wazi kuwa katika mechi hiyo hataangalia majina makubwa ya wachezaji, lakini ubora wa wachezaji.

Pacome amesema kuwa anataka mashabiki wa Yanga wafurahie kipaji chake na kwa kuanzia anataka kuanza na mchezo wa Agosti 8 dhidi ya Simba.

Ameeleza kuwa licha ya ushindani wa namba ndani ya timu kuwa mkubwa, lakini anataka kuwa na kitu tofauti ili kuhakikisha kwamba anapata nafasi na kufanya makubwa.

“Mchezo dhidi ya Simba utakuwa mgumu kutokana na wapinzani wao, kwani wamesajili wachezaji wazuri wenye ubora na rekodi za maana walikotoka.

Lakini sisi kama wachezaji tunatambua umuhimu wa matokeo mazuri kwenye mchezo mkubwa kama huo kwa kipindi cha mwaka mmoja nilichokuwa ndani ya Yanga.”

Ikumbukwe kuwa Pacome ni miongoni mwa wachezaji waliocheza mechi za Derby msimu uliopita baada ya kuwafunga Simba mabao 7-2 katika mechi mbili.

Licha ya rekodi hiyo, Yanga inaingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa na Simba ambayo ndiyo bingwa mtetezi wa Ngao ya Jamii.

Hata hivyo, msimu uliopita haukuwa mzuri kwa nyota huyo licha ya kufunga mabao saba na asisti nne, kwani majeraha yalimfanya kushindwa kucheza mechi mbili muhimu za robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns.

SOMA NA HII  HII HAPA REKODI YA SIMBA NA YANGA...HAIJAVUNJWA KWA MIAKA 45...MSUVA NA SAMATTA WASALENDA