Home news KUELEKEA MICHUANO YA CAF…SIMBA WAPIGWA MKWARA MZITO…WAAMBIWA WAJIANGALIE…

KUELEKEA MICHUANO YA CAF…SIMBA WAPIGWA MKWARA MZITO…WAAMBIWA WAJIANGALIE…


Siku moja baada ya kupangwa makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika huku Simba SC ikiangukia Kundi D, Kocha Mkuu wa klabu ya US Gendarmerie Rationale ya Niger, Zakariou Ibrahim amefunguka na kuwatumia salamu Mabingwa hao wa Tanzania Bara.

US Gendarmerie Rationale ya Niger, imepangwa kundi moja na Simba SC ya Tanzania, RS Berkane na Asec Mimosa ya Ivory Coast.

Simba SC itacheza dhidi ya US Gendarmerie Rationale Februari 20 mjini Niemy nchini Niger.

Zakariou Ibrahim amesema kuwa hatishwi na uzoefu na historia ya Simba SC, RS Berkane na Asec Mimosas katika mashindano ya klabu Afrika na anaamini vijana wake watapambana kuhakikisha wanamaliza katika nafasi mbili za juu kwenye kundi hilo ambazo zitawafanya watinge hatua ya Robo Fainali kwa mara ya kwanza katika historia ya timu hiyo.

Ametamba kuwa mkakati wao ni kutinga hatua ya Robo Fainali kupitia kundi hilo, na nafasi moja iliyobakia igombaniwe na timu nyingine kwenye Kundi D.

“Tupo katika kundi lililopangwa vizuri lenye timu tatu kubwa ambazo ni Berkane iliyowahi kutwaa taji hili, Simba ambao wamekuwa wakicheza vyema katika Ligi ya Mabingwa pamoja na Asec Mimosas ambao wamekuwa wakishiriki mashindano haya.”

“Malengo yetu ni rahisi tu, kumaliza tukiongoza na kufuzu hatua ya robo fainali. TRunaweza kufanya hivyo. Tunatakiwa kurudi katika mstari na kujituma pasipo kudharau taarifa yoyote muhimu,” amesisitiza kocha huyo wa Gendarmerie.

Katika Kundi hilo D, Gendarmerie pekee ndiyo ambayo haijawahi kufanya vizuri wala kuwa na uzoefu wa mashindano ya kimataifa kulinganisha na RS Berkane, Simba SC na Asec Mimosas.

RS Berkane iliwahi kutwaa taji la Shirikisho Afrika msimu wa 2019/2020 na msimu wa 2018/2019 ilifika hatua ya fainali wakati Asec Mimosas imewahi kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 1998.

Simba nayo japo haijawahi kutwaa taji la lolote la mashindano ya klabu Barani Afrika, mara kadhaa imekuwa ikifika hatua za juu za mashindano hayo, huku mwaka 1993 ikitinga hatua ya fainali ya Kombe la CAF ambapo ilipoteza mbele ya Stella Abidjan kwa kichapo cha jumla cha mabao 2-0.

SOMA NA HII  PABLO - TUTACHEZA SOKA 'BIRIANI' KESHO...AINGIA 'UBARIDI' DHIDI YA WAARABU...