Home Uncategorized NAFASI YA CIOABA YAGOMBEWA KAMA NJUGU AZAM FC

NAFASI YA CIOABA YAGOMBEWA KAMA NJUGU AZAM FC

UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa umepokea barua nyingi za maombi ya kazi kutoka kwa makocha mbalimbali duniani wanaotaka kubeba mikoba ya Kocha Mkuu Arstica Cioaba.

Cioaba kwa sasa yupo nchini Romania kwa ajili ya mapumziko ambayo yametolewa na Serikali baada ya kusimamisha Ligi Kuu Bara kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona, mkataba wake unakarabia kumeguka hivi karibuni.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zaka Zakazi amesema kuwa wamekuwa wakipokea barua nyingi kutoka kwa makocha mbalimbali wakiomba kukinoa kikosi cha Azam FC.

“Mkataba wa Cioaba unakarabia kuisha lakini kutokana na ukubwa wa Azam FC tumekuwa tukipokea barua nyingi za makocha ambao wanaomba kuifundisha Azam FC.

“Bado tunahitaji huduma ya Cioaba kwani yupo na timu kwa amekuwa na mafanikio hivyo ni suala la kusubiri,” amesema.

SOMA NA HII  VPL:SIMBA 3-0 IHEFU