Home Uncategorized KUMEKUCHA, KIUNGO MWINGINE NDANI YA SIMBA APIGIWA HESABU NA TP MAZEMBE

KUMEKUCHA, KIUNGO MWINGINE NDANI YA SIMBA APIGIWA HESABU NA TP MAZEMBE


JONAS Mkude iwapo mambo yatakuwa sawa huenda msimu ujao akasepa ndani ya Simba na kwenda kukipiga ndani ya Klabu ya TP Mazembe ya Congo.

Huyu atakuwa ni nyota wa pili ndani ya Simba kutakiwa na timu kubwa ikiwa ni baada ya kiungo Clatosu Chama kuelezwa kuwa anahitajika na Yanga.

Habari zinaeleza kuwa mabosi wa TP Mazembe wamekuwa wakimfuatilia kiungo huyo mkabaji ambaye ni kipenzi cha makocha wote ambao huwa wanatua ndani ya Simba kutokana na kucheza kwa umakini ndani ya uwanja.

Kabla ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa, Mkude alikuwa ametupia mabao mawili na kutoa pasi mbili za mabao jambo ambalo linazidi kumpadisha chati.

Mkude mwenyewe kuhusu dili hilo amesema:”Bado sijapata taarifa kuhusu suala hilo ni habari njema lakini ikiwa ni kweli basi taratibu za usajili zifuatwe,” amesema.

Hivi karibuni, Mtendaji Mkuu wa Simba,Senzo Mazingisa alisema kuwa miongoni mwa wachezaji bora ndani ya Simba ambao wanaweza kucheza soka la ushindani ni Mkude na itawezekana iwapo ataacha mambo ya nje ya uwanja.

“Mkude ni mchezaji mzuri na ana nafasi ya kucheza nje ya nchi na kwenye soka la ushindani ila inaweza kuwa rahisi kwakwe iwapo ataacha mambo ya nje ya uwanja,”.

SOMA NA HII  FRIENDS RANGERS YAKUBALI MUZIKI WA YANGA, SIBOMANA APEWA SALUTI