Home Uncategorized FRIENDS RANGERS YAKUBALI MUZIKI WA YANGA, SIBOMANA APEWA SALUTI

FRIENDS RANGERS YAKUBALI MUZIKI WA YANGA, SIBOMANA APEWA SALUTI

ELLY Mzozo, Kocha Mkuu wa kikosi cha Friends Ranger ya Morogoro amesema kuwa wachezaji wa Yanga wana ukomavu mkubwa na msimu ujao wataleta ushindani.

Friends Ranger leo imepoteza mchezo wa kirafiki mbele ya Yanga kwa kufungwa mabao 2-0 mchezo uliochezwa uwanja wa Highland Park Moro.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mzozo amesema kuwa kikosi cha Yanga kimeonyesha ushindani mkubwa na ukomavu wa kipekee.

“Wachezaji wameonyesha juhudi na wanajituma kiukweli ndio maana wamepata matokeo, nyota kama Sibomana ameonyesha uwezo na spid hivyo ni matumaini yangu kwamba ataleta ushindani akiyazoea mazingira.

“Siri kubwa ya mchezaji inabebwa kwenye namna anavyocheza na mpira akiwa ndani ya uwanja hivyo tutashuhudia mengi msimu ujao,” amesema.

SOMA NA HII  MAAMUZI YA MORRISON KUTOLEWA LEO KUHUSU ISHU YA MKATABA WAKE