Home Habari za michezo SIMBA NA YANGA WAONYWA KUACHA USHIRIKINA.

SIMBA NA YANGA WAONYWA KUACHA USHIRIKINA.

habari za simba na yanga

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almas Kasongo amesema katika kanuni mpya za ligi faini ya kuhusu ushirikina imeongezeka pia lakini wataendelea kutoa Elimu ili vilabu viache haya kwani inachafua ligi.

Vilabu vinavyotajwa kwenye   suala  hili la ushirikina sio tu timu ndogo, bali hata Simba na Yanga wamekuwa mstari wa mbele kuonesha vitendo hivyo vichafu tena hadharani.

Akizungumza jana wakati wa maandalizi ya Msimu mpya wa 2024/25,  Kasongo alisema mwaka jana timu nyingi zilizonesha vitendo   vya ushirikina hadharani, hivyo hiyo  iliitia doa ligi kuu.

“Bodi tumekaa na Wenyeviti wa timu tukubaliana tuongeze faini kwa timu zinaonyesha vitendo vya kishirikina, maana msimu uliopita kanuni hii ilivunjwa zaidi na timu zinalipa faini lakini hata hawajali, tulijiuliza faini ilikuwa ni ndogo,” amesema Kasongo.

Kwa kuliona hilo na kutambua ubora wa Ligi kuu ya  Tanzania vitendo vya Ulozi, havitakiwi katika timu zote zinazoshiriki kwani vinatengeneza picha  mbaya huku nje.

Kwa nyakati tofauti vilabu vikibwa ikiwemo Simba na Yanga, vimepigwa faini kwa kuonesha vitendo vya ushirikina,  kwa kushikilikisha wachezaji, mashabiki au viongozi.

SOMA NA HII  VITA YA SIMBA NA YANGA IMEANZA UPYAA