Home Habari za Simba Leo FADLU KUELEKEA MECHI YA YANGA…ANATAKA USHINDI TU

FADLU KUELEKEA MECHI YA YANGA…ANATAKA USHINDI TU

Habai za Simba- Fadlu

KOCHA Mkuu wa Simba Fadlu Davids amezungumzia mchezo wa kesho dhidi ya Yanga, na kusema kwamba hauchukulii mchezo huo kawaida bali anhitaji ushindi tu.

Fadlu ameyasema hayo leo katika kikao na Waandishi wa Habri kuelekea mchezo wa Kariakoo Dabi, Nusu fainali utakaopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa majira ya Saa 1:00 Usiku.

“Tunavipaji vingi kwenye timu na tunaendelea kujenga umoja tunachukua mchezo huu kama michezo mingine na hatuna presha.

“Tunaingia kucheza kwa ajili ya kushinda na ni mchezo utaotupa picha ya kuelekea msimu ujao nimi cha kufanya zaidi ?

“Hii ni timu mpya na project mpya mechi tulizocheza zinaendelea kutujenga na taratibu tutaendelea kuimarika

Hatuwezi kuzuia muda wote wala kushambulia muda wote lakini tutatengeneza mpango ambao tutaweza kushinda” Amesema Kocha Mkuu wa Simba- Fadlu

Mchezo huo unatazamwa kwa jicho la kipekee zaidi kwa mashabiki wa Simba, ambao msimu uliopita walipokea kipigo mara mbili, jumla ya mabao 7, hivyo wanahitaji kurejesha heshima yao iliyopotea.

SOMA NA HII  JE SIMBA WATAENDELEZA UBABE LEO!?