Home Habari za Yanga Leo AZAM FC WATANGAZA KUACHANA NA PRINCE DUBE…ANUKIA ZAIDI YANGA

AZAM FC WATANGAZA KUACHANA NA PRINCE DUBE…ANUKIA ZAIDI YANGA

HABARI ZA YNGA

UONGOZI wa Azam FC wametangaza kuachana na aliyekuwa mchezaji wao Prince Dube ambaye alikuwa kwenye mgogoro wa kimkataba na miamba hao wa Chamazi.

Kupitia kwenye taarifa ya klabu hiyo ilielezea namna ambavyo Azam FC imepokea fedha ambazo mchezaji huyo alitakiwa kulipa ili kuvunja mkataba wake.

“Tunapenda kuutarifu umma kwamba tumeridhia maombi ya Prince Dube kuvunja mkataba wake nasi, aliyoyatoa Machi 2024.

“Hatua hii inafuatia kitendo cha mchezaji huyo kutimiza matakwa ya kimkataba kama ilivyoainishwa kwenye vipengele vinavyoruhusu upande mmoja kuvunja mkataba”

“Tunamtakia kila la kheri katika safari yake ya soka na maisha kwa ujumla.” Iliandika taafifa hiyo.

Prince Dube alikuwa kwenye mgoogoro mkubwa na waajiri wake wa zamani klabu ya Azam FC, baada ya kujivunjia mkataba mwenyewe, hali iliyowapelekea viongozi wa timu hiyo kwenye kamati ya usuluhishi wa TFF.

Dube alianza kwa kurudisha kila kitu cha Azam FC, ikiwemo gari na nyumba aliyopewa kuishi, lakini mgogoro huo ulienda mbali zaidi na TFF kumtaka mchezaji huyo kulipia fidia ya kuvunja mkataba wake.

Mchezaji huyo ambaye alidumu kwenye klabu hiyo kwa misimu miwili hajawahi kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu hata kwa msimu mmoja, anapea nafasi kubwa ya kusajiliwa na Yanga ambao kwa muda mrefu walikuwa wanahitaji saini ya mshambuliaji huyo wa Kimataifa wa Zimbabwe.

SOMA NA HII  MECHI YANGA VS TP MAZEMBE...AZIZ KI,AUCHO NA DIARRA WAPIGWA CHINI