Home Habari za Simba Leo JOHN BOCCO KUFANYA SAPRIZI KABLA YA SIMBA DAY

JOHN BOCCO KUFANYA SAPRIZI KABLA YA SIMBA DAY

HABARI ZA SIMBA

Muda wowote kuanzia sasa John Bocco, atatangazawa kama mchezaji mpya wa JKT Tanzania. Moja ya sapraizi ambayo mashabiki wa Simba hawakuitarajia kwani walishampa ukocha kwenye timu yao ya vijana baada ya kumstaafisha kwa heshima.

Taarifa za ndani kutoka kwa uongozi wa JKT, kuwa Bocco ndiye atakayekuwa nahodha mpya wa kikosi hicho.

Bocco amesajiliwa JKT Tanzania kwa mkataba wa mwaka mmoja, baada ya Simba kumpiga chini, licha ya kwamba alipewa majukumu mengine ya kukinoa kikosi cha vijana wenye umri chini ya miaka 17, ameachana nayo na kukubaliana na dili la kurudi kucheza uwanjani.

“Bocco tutampa heshima ya kuwa nahodha, ndio maana tumemsajili kama kocha mchezaji, tunaamini bado ana uwezo uwanjani, pia ana vitu vya ziada atakavyowasaidia wenzake kuwaongoza,” alisema.

Nje na Bocco, Mwananchi linafahamu kwamba Said Ndemla na David Bryson baada ya kumaliza mikataba yao ya mkopo, wamepewa mikataba mipya, hivyo wataendelea kuwa sehemu ya kikosi hicho msimu ujao.

“Ndemla na Bryson walikuwa wanacheza kwa mkopo kutoka Singida FG, kwa sasa tumewasainisha mikataba mipya kama wachezaji huru,” alisema.

Mbali na hao, mshambuliaji Charles Ilanfya aliyeshuka na Mtibwa Sugar, imeelezwa pia amejiunga na kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao.

Simba iliachana na John Bocco akiwa ni mchezaji wa kwanza kabisa kumpa Thank You, wakati  wakijiandaa na kuwaacha wengine JKT Tanzania wamepita nae, hii inatoa taswira ya kwamba Bado Anaona anafaa kuwa uwanjani kama mchezaji na sio kocha.

SOMA NA HII  SIMBA NA YANGA ZAIPANDISHA VIWANGO TANZANIA KISOKA...YAPANDA NAFASI TATU CHAP