Home Habari za michezo YANGA YAZIPIKU SIMBA, AZAM FC UPIGAJI MASHUTI…YASUBIRI TUZO ZA TFF

YANGA YAZIPIKU SIMBA, AZAM FC UPIGAJI MASHUTI…YASUBIRI TUZO ZA TFF

Hbari za Yanga leo

KLABU ya Yanga msimu wa 2023/24 umekuwa mzuri sana kwa upande wao baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa wa 30 wa Ligi Kuu, huku ikiweka rekodi ya kuwa kinara wa kupiga mashuti mengi yaliyolenga lango “shout on target”, ikizipiku tena Simba SC na Azam FC ambao wao wanaongza kwa kupiga mashuti yasiyolenga lango “off target”

Kwa mujibu wa Bodi ya Ligi, Yanga imepiga mashuti 205 ambayo yamelenga lango, ikiwa ndiyo timu iliyoongoza kufanya hivyo, ikifuatiwa na Azam FC, ambayo mashuti yake 196 yalilenga, huku Simba ikishika nafasi ya tatu, ikiwa na mashuti 177 yaliyolenga lango.

VILAVU VINGINE VYA LIGI KUU.

Tabora United, ndiyo iliyopiga mashuti machache yaliyolenga lango, ikifanya hivyo mara 93 tu, ikifuatiwa na Coastal Union mara 96, na Geita Gold ikipiga mara 99.

MASHUTI YASIYOLENGA LANGO “OFF TARGET”

Kwa mashuti yasiyolenga lango, Azam FC ndiyo kinara, ilipiga mashuti 220, ikifuatiwa na Mtibwa Sugar iliyopiga mashuti fyongo mara 209, Yanga ya tatu ilipiga makombora 192, huku Mashujaa FC ikipiga mashuti machache zaidi yaliyotoka nje, ikifanya hiyo mara 125.

MABEKI WALIOKOA HATARI NYINGI.

Takwimu zinaonesha kwamba mabeki wa Coastal Union ndiyo waliookoa hatari nyingi zaidi langoni mwao msimu huu, ikifanya hivyo mara 334, Mashujaa FC na Prisons zikiondoa hatari langoni mwao mara 321.

Mabeki wa Yanga wameokoa hatari chache zaidi katika ligi hiyo iliyomalizika, wakifanya hivyo mara 157, wakifuatiwa na wa Simba wakiokoa mara 177. Hi ina maana kwamba timu hizi hazikuwa zikishambuliwa kiasi hicho.

Ihefu FC, kwa mujibu wa takwimu kutoka Bodi ya Ligi, ndiyo timu ambayo viungo wao wa kati walizuia hatari nyingi kuelekea langoni mwao.

Waliharibu mpango ya wapinzani na kunasa mipira mara 491, wakifuatiwa na Prisons mara 445, KMC mara 441, huku viungo wa JKT Tanzania wakishika nafasi ya mwisho kwa kunasa mipira ya wapinzani, wakifanya hivyo mara 331, wakifuatiwa na Tabora United, mara 333.

SOMA NA HII  GEITA GOLD WANOGEWA NA DUCHU...MIKAKATI YAFANYWA KIMYA KIMYA KUEPUSHA SHARI ZA SIMBA NA YANGA...