Home Habari za michezo SIMBA KUVUTA ‘MDAKA MISHALE’ WAO KUTOKA BURUNDI….JAMAA ANADAKA MPAKA HEWA…

SIMBA KUVUTA ‘MDAKA MISHALE’ WAO KUTOKA BURUNDI….JAMAA ANADAKA MPAKA HEWA…

Tetesi za Usajili Simba

SIMBA imeliweka mezani jina la kipa wa Coastal Union ya Tanga, Justin Ndikumana raia wa Burundi, ikijadili kiwango chake kama kinaweza kuongeza nguvu msimu ujao, wakati huo huo Singida Big Stars na Geita Gold nao wanahitaji huduma ya mchezaji huyo.

SBS na Geita zimechukua hatua ya kuzungumza na waajiri wa kipa huyo (Coastal), kujua ana mkataba wa muda gani ili wajue kama wanaweza wakauvunja au la.

Ndikumana alisaini mkataba wa miaka miwili ndani ya kikosi hicho, akitokea Bandari ya Kenya, kwa muda mfupi ameonyesha kiwango cha juu.

Chanzo cha ndani kutoka kwa kiongozi mmoja wa Simba, kilisema “Ndikumana ni kati ya majina yaliopendekezwa kusajiliwa kutokana na kiwango alichokionyesha kwa muda mfupi akiwa na timu yake ya Coastal.

Kiliendelea kusema; “Lazima atafutwe kipa mzoefu wa kuziba nafasi ya Beno Kakolanya aliyesaini timu nyingine, ukiachana na hilo, Aishi Manula anaumwa anaweza akakaa muda mrefu nje.”

Tangu ajiunge nao dirisha dogo, amecheza mechi saba dhidi ya dhidi ya Kagera Sugar 0-0,Geita 1-0 Coastal, Coastal 1-0 Prisons, Coastal 1-0 Mbeya City, Coastal 1-1 SBS, Dodoma Jiji 1-1 Coastal, Coastal 1-0 Mtibwa Sugar, amefungwa mabao matatu ana krinishiti nne.

Alipotafutwa kipa huyo kujua kama ametafutwa na viongozi wa klabu zinazotajwa kumtaka alisema “Naheshimu mkataba wangu, hivyo siwezi kuzungumza chochote kwa sasa, kama zinamanisha zitawatafuta mabosi wangu, nina uzoefu kwani nimecheza miaka tisa nje ya nchi yangu ya Burundi .”

Kwa upande Coastal Union, Msemaji Jonathan Tito alisema “Zipo timu nyingi zinazohitaji saini ya kipa huyo, lakini itakayokuwa inamanisha itazungumza na uongozi, maana bado ana mkataba na sisi.”

SOMA NA HII  HAYA HAPA YA KUZINGATIA KWA SIMBA NA YANGA ILI WATOBOE CAF ....WAKIFELI NI AIBU KWA NCHI...