KOCHA wa Yanga, Miguel Gamondi ametuma ujumbe kwa viongozi na wachezaji bila kujali wale wapya ambao wanatajwa kusajiliwa Prince Dube, kiungo Clatous Chama kila mmoja anatakiwa kufanya hivyo.
Ujumbe ambao Gamondi ameutuma kisha fasta mabosi wa Yanga kuufikisha kwa mastaa hao ni kila mchezaji anatakiwa ahakikishe ikifika Julai Mosi awe hapa nchini kuanza maandalizi ya kuelekea msimu mpya.
Yanga itaanza kambi mpya Julai Mosi mwaka huu ambapo kila mchezaji na benchi la ufundi linatakiwa liwe limefika kambini.
Klabu hiyo inahusishwa zaidi na usajili wa mshambuliaji Prince Dube, na kiungo wa Simba Clatous Chama ambao wate kwa pamoja wanapewa nafasi kubwa ya kucheza timu moja msimu ujao.
Dube inaelezwa tayari amemalizana na klabu ya Azam kwa kuwalipa pesa zao, huku akiwa bado na deni lililobaki, hivyo ili kujiunga na Yanga inahitajika busara za Uongozi wa Azam FC kuruhusu usajili wake ukamilike.
Upande wa Kiungo Chama anamaliza mkataba wake na Simba Tarehe 30 Juni, hivyo kinachosubiriwa kwa sasa ni upande wake mchezaji kama atakubali kuongeza mkataba mpya na klabu yake ya sasa, au kama hataki basi anapewa nafasi kubwa sana ya kuinasa saini ya mchezaji huyo wanayemtamani kwa kipindi kirefu.
Huenda ile ndoto ya mashabiki na wapenzi wa Yanga ya kumuona Chama akiwa na uzi wao itaenda kutimia msimu ujao, muda ni hakimu mzuri zaidi.