Home Habari za Yanga Leo BREAKING NEWS…YANGA YAFUNGIWA KUSAJILI, SABABU ZAWEKWA WAZI

BREAKING NEWS…YANGA YAFUNGIWA KUSAJILI, SABABU ZAWEKWA WAZI

Habari za Yanga leo

KLABU YA YANGA imefungiwa kusajili wachezaji wapya, kutokana na kukiuka kanuni za usajili za FIFA.

Taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu TFF, iliyotoka leo Jumanne Juni 18, imevitaka vilabu vyote vinayodaiwa na wachezaji wao kuwalipa haraka.

Yanga ni moja ya timu 5 ambazo zimefungiwa na FIFA kusajili, ambapo tayari dirisha la usajili limefunguliwa tangu Juni 15, lakini taarifa ya FIFA inakuja muda mfupi tangu klab hiyo ya Yanga ifungiwe tea kusajili mwezi April kutokana na kutokamilisha usajili wa mchezai wake kwenye mfumo wa FIFA.

Taarifa ya TFF iliandika kwamba; “Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) pamoja na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imezifungia klabu zifuatazo kusajili mpaka zitakapowalipa wachezaji wanaozidai”

“Klabu ambayo itawalipa wahusika, itaondolewa mara moja adhabu ya kufungiwa kusajili hadi leo asubuhi kupitia mfumo wa FIFA (FIFA Legal portal) hakuna taarifa ya klabu yoyote kati ya hizo iliyowalipa wahusika”

Timu zilizofungiwa kusajili ni Young Africans SC (Yanga), Singida Fountain Gate FC (kwa sasa Singida Black Star)c, Tabora Utd iliyosalimika na kushuka daraja baada ya kucheza Play Off, Biashara Utd ya Mara, FGA Talents FC.

Inasemekana mchezaji anayeidai Yanga ni Hafiz Konkoni ambaye alivunjiwa mkataba wake kwenye dirisha dogo na nafasi yake kusajilliwa Joseph Guede,  ambaye kwa sasa ameonekana kuwa na makali kenye eneno la ufungaji.

SOMA NA HII  KUHUSU PITSO NA IBENGE KUHUSISHWA NA YANGA ...UKWELI WA MAMBO HUU HAPA...LOLOTE LINAWEZEKANA...