Home Habari za Yanga Leo MAPYA YAIBUKA UJENZI UWANJA WA YANGA…INJINIA HERSI AFUNGUKA UKWELI

MAPYA YAIBUKA UJENZI UWANJA WA YANGA…INJINIA HERSI AFUNGUKA UKWELI

Habari za Yanga- Injinia Hersi

RAIS wa Yanga, Injinia Hersi Said amesema kuhusu mipango ya kujenga uwanja wao wa kisasa katika eneo la Jangwani, walipewa machaguo mawili, walipwe fidia na kuhama katika eneo hilo ambalo liko katika mipango ya kuboreshwa au wajenge uwanja ulio bora kabisa.

Aliyasema hayo jana alipokuwa akihutbia wanachama na mashabiki wa timu hiyo, katika mkutano mkuu wa mwaka, ambapo ulihusiana na ukaguzi wa hesabu za matumizi kwa msimu   mzima, na kupitisha bajeti kuu ya klabu hiyo  mwaka 2024/25 ambayo  inafikia Bilioni 24 za kitanzania.

“Serikali ilitufanya tuchague mambo mawili, kuachia uwanja ili turudishiwe fidia ama kujenga uwanja wa kisasa utakaoendana na eneo hilo, tulichagua namba mbili na sasa naamini Yanga itakuwa na uwanja wa kisasa hapa nchini.”

“Tunamshukuru mzee wetu aliyetangulia mbele ya haki, Abeid Amani Karume aliyejenga jengo hilo mwaka 1971, lakini kila kitu kinatakiwa kufanyiwa marekebisho na sasa Yanga ndio iliyo na jengo la kisasa kuliko klabu zote Tanzania na kama siyo Afrika.

Mbali na hilo, alizungumzia msimu ujao (2024/25), kwamba watakuwa na msimu bora kuliko uliopita.

“Msimu bora unaanzia na usajili, tutakuwa na benchi bora kuliko la msimu uliopita, tutakuwa na wachezaji bora, kila mwaka tutaongeza wachezaji wenye ari na mafanikio, hatuwezi kubweteka kutokana na mafanikio tuliyopata, tutakuwa na kambi nzuri, tumealikwa Iran, Afrika Kusini na Kenya kufungua uwanja wao mpya wa kisasa,” alisema.

Kwa kauli ya rais wa Yanga ni kama inakoleza moto wa kocha wao Muargentina, Miguel Gamondi ambaye bado hajasaini mkataba mpya na tetesi nyingi zinamzunguka ikiwamo kutakiwa na klabu nyingine.

SOMA NA HII  AHMED ALLY AWACHANA CHAMA,MANULA NA KAPOMBE...PUNGUZENI MAKOSA,TUMIENI NAFASI...AMPIGIA SALUTI KIPA VIPERS