Home Habari za Simba Leo MO DEWJI AWAJIA JUU WANAOTAKA AONDOKE SIMBA…ONA ALICHOSEMA

MO DEWJI AWAJIA JUU WANAOTAKA AONDOKE SIMBA…ONA ALICHOSEMA

Habari za Simba- Mo Dewji

Rais wa Heshima na Mwekezaji wa Simba SC, Mohammed  Dewji “MO” ameibuka kwa  nguvu sana mitandaoni, na kuwafanya mashabiki  wa timu hiyo kufikiria mambo mengi juu ya kinachoendelea ndani ya klabu yao.

Simba imekuwa katika sintofahamu kwa kipindi cha siku tatu mfululizo, huku wajumbe wa bodi upande wa wanachama wakifichua namna wanavyopata wakati mgumu wa kuafiki mawazo ya Mo katika uwekezaji wa klabuni hapo.

Wikiendi hii imekuwa na heka heka mitandaoni na kwa mashabiki wa Simba baada ya Mo Dewji kuandka katika ukurasa wake instagram ujumbe unaosomeka: Kujikwa si kuanguka, bali ni kwenda mbele. Simba Tupo Pamoja!

Lakini pia kupitia insta stori yake MO Dewji aliposti wimbo wa msanii Tunda Man “Tambeni” ukituma ujumbe wa kwamba “Mtanipiga mpaka mniue mimi Simba Sihami”

Bila shaka MO Dewji anajaribu kuwaambia mashabiki kile kinachoendelea ndani ya klabu hiyo kwa sasa, kitu ambacho kinaifanya timu hiyo kushindwa kupiga hatua zaidi.

Taarifa tulizozinyka zinaeleza kwamba, kuna nguvu inatumika kubwa tu ya kumkwamisha muwekezaji ili aondoke klabuni hapo,  na timu apewe kigogo mmoja (Jina linahifadhiwa) Soka LA Bongo tunaendelea kufuatilia ukweli wa taarifa hizi, endapo tukizipata utakuwa wa kwanza kuzipata, endelea kuwa nasi.

Hapa ni kwa waliosoma CUBA tu! Ujumbe wa MO Dewji ni kama majibu ya kilichoelezwa siku Jumamosi na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Issa Masoud alifafanua kuhusu Sh20 bilioni zilizopaswa kuwekwa na mwekezaji huyo, akisema Mo anataka kugeuza fedha ambazo amekuwa akizitoa kwa klabu kama msaada kuwa deni au zigeuzwe mtaji.

Akizungumza na waandishi wa habari, Masoud alisema walipokea taarifa ambazo hazikuwa katika urasmi wake ikiwataka kama bodi kupitisha azimio lililokuwa likisema pesa alizokuwa anazitoa mwekezaji kama msaada zihesabiwe katika hisa.

Hata hivyo, ujumbe wa Mo Dewji ulipokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo wengine wakimuunga mkono kwa kaulio hiyo wakisema wapo pamoja naye na wengine wakimpiga ‘dongo’ kiaina.

SOMA NA HII  COASTAL WAMKATAA MGUNDA KWEUPE...SABR AELEZA