Home Habari za Simba Leo MHE HAMIS KIGWANGAlLA AMJIA JUU MO DEWJI…SIMBA INAKUDAI PESA NYINGI

MHE HAMIS KIGWANGAlLA AMJIA JUU MO DEWJI…SIMBA INAKUDAI PESA NYINGI

Habari za Simba, Kigwangalla na Mo Dewji

WAKATI ambao Muwekezaji wa Simba Mohamed Dewji MO akipanga mipango ya msimu ujao, akiwa ameanza na wajumbe wake kuwataka wajiuzulu, kumeibuka mambo mengi na habari nyingi kutoka kwa baadhi ya wananchama wa timu hiyo kumshtumu MO Dewji kuwa haidai Simba bali Simba ina mdai.

Siku y Jana Soka la Bongo tuliripoti uwepo wa kikao cha wanachama wa matawi na baadhi ya wajumbe wa Simba, baada ya kikao miongoni mwa mamabo yaliyozungumzwa sana ni madai  ya MO Dewji kuwa anaimiliki Simba, huku CPA Issa Masoud akiweka wazi kwamba MO Dewji hakuwahi kuipa Simba zile Bilioni 21, za kwenye mchakato.

Sasa Mhe Hamis Kigwangalla nae katika ukurasa wake Instagram aliandika ujumbe huu kwenda kwa Muwekezaji MO Dewji, Mwenyekiti wa Simba Murtaza Mangungu na Wanachama na Mashabiki wa timu hiyo.

“Kama ni kudaiana tu, tena bila mikataba, basi na sisi Wana SimbaSC tunamdai mwekezaji pesa nyingi sana!”

“Tulimtaka aweke bilioni 20 kwenye akaunti yetu ili tununue bonds, kumbe hakuweka! Kama angeweka tungenunua bonds za miaka 25, at a coupon rate of 15.95% tungepata faida ya bilioni 3.19 kila mwaka. Kwa miaka 7 aliyotuzubaisha bila mafanikio yoyote yale, tungevuna bilioni 22.33!

“Deni la pili: ni pesa alizotukosesha kutokana na ufadhili wa Azam Media – bilioni ngapi? Kwa mwaka ni bilioni 3. Kwa miaka 7 ni bilioni 21!

“Na yeye matangazo yake alikuwa analipia ufadhili kiasi gani?

“Tayari kwa haya mawili tu, tunamdai mwekezaji Glezabhai zaidi ya bilioni 43.33! Taja na wewe madeni mengine tunayomdai Glezabhai ili twende sawa!

“Halafu, Wajumbe wa Bodi waliokurupuka leo kutoka usingizini tuna jambo nao: watuambie walimpa Glezabhai mamlaka ya kumiliki timu yetu kwa msingi upi? Maana hakufuata prospectus ya mchakato wa transformation wa kampuni inavyotaka.

“Nimemuona Ndugu Issa akitumia Memorandum ya kampuni…how? Kama mchakato wa kulipia hisa haujakamilika hiyo document haina nguvu yoyote ile, ile bodi yao waliyokuwa wanakaa haina maana yoyote ile. Na wala Simba Sports Club haijauzwa na wala haidaiwi na mtu – kimsingi tumerudi GROUND ZERO!

“Ile bodi ilikuwa genge la watu walioiteka tu timu yetu kinyemela. Kwa taarifa za Ndg. Issa Masoud, maana yake Glezabhai hana haki wala mamlaka yoyote yale kisheria kwenye Simba. Simba SC ni club ya wanachama kwa asilimia 100.

“Wanachama tunamtaka Ndg. Mangungu aitishe mkutano mkuu haraka tuamue hatma ya club yetu. Kwenye mkutano huo aandae hesabu za mapato na matumizi ya Simba….kuanzia viingilio vya getini siku za mechi, mikataba ya mauzo ya bidhaa, mikataba ya mauzo ya haki za matangazo (ikiwemo ya bidhaa za Glezabhai, mbet nk), mapato ya CAF (robo fainali zote), n.k.

“Ndg. Mangungu na Kamati Tendaji wakishindwa kufanya hivi, tutaingilia kati kwa kuunda ‘kikosi kazi’ maalum (task force) cha kuiokoa club yetu.”

SOMA NA HII  PAMOJA NA MKUDE KUAGWA 'KIBABE' JANA.... 'VIBE' LA SIMBA DAY YA JANA ILIANZIA HUKU KUMBE....