Home Habari za Yanga Leo MSIGWA ATABIRI MAKUBWA YANGA…ITAFIKA LEVEL ZA MAN UTD, ARSENAL

MSIGWA ATABIRI MAKUBWA YANGA…ITAFIKA LEVEL ZA MAN UTD, ARSENAL

Habari za Yanga leo

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa akimwakilisha waziri, Damas Ndumbaro katika mkutano mkuu wa mwaka wa Yanga 2024, amesisitiza juu ya weledi katika namna ya uendeshaji kwa klabu za Ligi Kuu Bara, huku akiilinganisha klabu hiyo kama vilabu vya Ulaya kma Arsenal, Manchester Utd.

Msigwa amesema hayo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam wakati akiwapongeza viongozi Yanga kwa mageuzi makubwa ambayo wameyafanya.

“Kwa niaba ya Waziri naomba kuwafikishia salamu kwa kuwapongeza kwa ubingwa wa 30, amewapongeza pia kwa ubingwa wa FA, ameniambia niwaambie yupo pamoja nanyi,” amesema Msigwa na kuongeza;

“Kwa dhati ya moyo wangu naomba kuwapongeza kwa mafanikio makubwa, upande wa wizara kwa niaba ya Serikali jambo muhimu ni namna Yanga mmetengeza weledi katika uendeshaji. Serikali tunatamani kuona klabu zikiwa na uendeshaji mzuri wa uendeshaji. Tunataka kuwa sehemu ya mafanikio na sio usuluhishi wa migogoro. Naiona Sayansi kwenye klabu ya Yanga.”

“Nawapongeza Yanga kwa Mafanikio mliyopata na mmeongeza weledi katika Uongozaji wa Timu nawaomba muendelee kufanya hivi ili wengine waige hii njia nzuri, sasahivi mmefika kwenye njia ya kuendesha Timu kama Manchester United, Arsenal na Timu zingine kubwa nasema haya sababu nimeonjeshwa kidogo na Hersi namna Mipango ya Yanga inavyofanyika”

Msigwa alimalizia kwa kuwataka Yanga kuendelea kuwa mfano mzuri juu ya namna ya uendeshaji wa klabu; “Kuna mahali mmesogea, natamani kuona klabu za Tanzania ifike hatua ziwe kiuendeshaji sawa na klabu kubwa za soka Ulaya.”

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe alisema katika mkutano huo mara baada ya katibu huyo kuongea kuwa viongozi wa TP Mazembe walikuja nchini kwa ajili ya kuangalia namna ya uendeshaji wa klabu hiyo kutokana na kufanya kwao vizuri.

Kauli hiyo ilikuwa ni kama majibu kwa Msigwa kuonyesha kile ambacho wanafanya kimeanza kuonekana na kuigwa na klabu nyingine za ukanda huu wa Afrika Mashariki.

SOMA NA HII  LILE DILI LA AZIZ KI KUTUA YANGA ...MPANGO MZIMA UKO HIVI....MANARA AANIKA MCHONGO WOTE ULIVYO...