Home Habari za Yanga Leo YANGA KUFANYA UMAFIA…JEAN BALEKE AFICHWA HOTELINI

YANGA KUFANYA UMAFIA…JEAN BALEKE AFICHWA HOTELINI

Habari za Yanga, Jean Baleke Yanga

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga wana jambo lao kubwa Juni 9 2024 ambapo ni Mkutano Mkuu wa Wanachama, (Annual General Meeting-AGM). Lakini tetesi ni kubwa zaidi kuhusu ujio wa nyota Jean Baleke katika klabu hiyo.

Inaelezwa kwamba moja ya suprizi iliyoandaliwa ni kuhusu taarifa za Aliyekuwa mchezaji wa Simba Jean Baleke, inasekana kwamba mabosi wa yanga wamemuita Tanzania, na sasa yupo hoteli moja posta, kama mambo yatenda sawa huenda ukawa ni usajili wa Yanga wa kwanza kwa msimu huu.

Yanga imkuwa ikiteseka sana kutafuta mtu katiri kwenye lango la wapinzani wao, lakini nafasi iliyoachwa na Fiston Mayele ni kama bado haijappata mtu sahihi.

Jean Baleke aliachwa na watani zao Simba, baada ya mkataba wake mkopo kumalizika na kutimkia Libya kwenye klabu ya Al Ittihad ambao msimu huu wametwaa taji la Ligi Kuu, sasa yupo kwenye mazungumzo ya kina zaidi na yanga lakini pia Azam FC wanahusishwa zaidi kumhitaji nyota huyo.

Yanga chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi Yanga imetwaa taji la Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 80 na ilitwaa taji la CRDB Federation Cup kwa ushindi dhidi ya Azam FC kwenye fainali iliyochezwa Juni 2 2024.

Ilikuwa ni Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar, dakika 120 ngoma ilikuwa Azam FC 0-0 Yanga na kwenye changamoto ya penalti ilikuwa Azam FC 5-6 Yanga langoni alikuwa ni Djigui Diarra kwa Yanga na Azam FC ni Mustapha Mohamed.

Kamati ya Utendaji ya Yanga chini ya Rais Hersi Said leo Juni 2024 ilifanya kikao maalumu kwa ajili ya maandalizi ya AGM)kilichofanyika katika ukumbi wa Urban By City Blue, Masaki Jijini Dar.

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika Posta, Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere ambapo hata ule uliopita 2023 ulifanyika hapo kwa wanachama waliokidhi vigezo kuhudhuria mkutano huo.

Taarifa rasmi kutoka Yanga imetaja baadhi ya matawi ambayo yamekidhi vigezo vya kushiriki yakiwa yameongezeka ikiwa ni pamoja na GSM Family, Yanga B.O.T, Yanga Alliance, Brotherhood VIP na Magomeni Makuti yote ya Dar.

SOMA NA HII  MIKWARA YA NGAO YA JAMII IMESHAANZA, BENO ATAMBA MBELE YA SIMBA