Home Habari za Yanga Leo PRINCE DUBE NI SUALA LA MUDA TU YANGA.

PRINCE DUBE NI SUALA LA MUDA TU YANGA.

Prince Dube Yanga

MABOSI wa Yanga SC wapo mbioni kukamilisha dili la kumsajili aliyekuwa mshambuliaji wa AZAM FC, Prince Dube ambaye katikati ya msimu alijivunjia mkataba na klabu yake, huku ikielezwa kwamba anahitajika na miamba hao.

Dube na Azam FC ilifikia hatua ya kufikishana hadi Kamati ya Haki za Wachezaji kwenye Shirikisho la Mpira wa Miguu TFF, ili kusikilizwa madai ya kimkataba baina ya pande hizo mbili.

Baada ya kamati ya TFF kusikiliza utetezi wa pande zote mbili, na ushahidi wa kimkataba waliamua kwamba Prince Dube alikuwa amekosea kwa mujibu wa mkataba wake na Azam FC, hivyo kama anahitaji kuondoka atatakiwa kulipa fidia za kimkataba na waajiri wake wa zamani.

Kabla ya sakata hili kufika TFF, Prince Dube alikuwa akihusishwa zaidi ya Yanga ambao hawakuwa na mshambuliaji kinara wa mwenye roho mbaya, kabla ya Joseph Guede kuanza kikiwasha na sasa Uongozi wa klabu hiyo chini ya Rais Eng Hersi wameanza kufanya mazungumzo ya kumsaini fundi huyo wa kufunga mabao.

Yanga ina amini kwamba Prince Dube ni mrithi sahihi wa Fiston Mayele, aliyeondoka msimu uliopita na kujiunga na Pyramids FC, na tangu aondoke Mayele eneo la ushambuliaji la Yanga lilikosa kiongozi sahihi.

Hii inadhihirishwa na suala la Aziz Ki kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu, na kiuchezaji sio namba 9, lakini wachezaji waliopo kwenye hiyo namba kama Clement Walid Mzize, na Joseph Guede aliyesajiliwa dirisha dogo wameshindwa kufua dafu kwa Aziz Ki.

Endapo Yanga watampata Prince Dube basi watakuwa wmaetibu tatazo la upachikaji wa magoli, kama mchezaji huyo atakuwa sawa bila majeraha ambayo yalikuwa yakimsumbua zaidi akiwa na waajiri wake wa zamani.

Prince Dube amekuwa akifanya mazoezi maeneo ya Avic Town kwa ulinzi mkali, tena chini ya uangalizi wa mabosi wa Yanga, kwa sasa inaelezwa yupo nchini kwaajili ya mazungumzo na mabingwa mara nyingi zaidi wa Ligi Kuu.

SOMA NA HII  YANGA YAWAFICHA MASTAA WAKE ULAYA...KUANZA KUTAMBULISHWA MUDA WOWOWTE